> Kutuma Faksi (Vichapishi vinavyotuma Faksi Pekee) > Kupokea Faksi kwenye Kompyuta

Kupokea Faksi kwenye Kompyuta

Faksi zinaweza kupokewa kwa kichapishi na kuhifadhiwa kwenye umbizo laPDF au TIFF kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi. Tumia FAX Utility (programu tumizi) ili kuunda mipangilio.

Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuendesha FAX Utility, tazama Basic Operations kwenye msaada wa FAX Utility (yanayoonyeshwa kwenye dirisha kuu). Iwapo skrini ya ingizo la nywila itaonyeshwa kwenye skrini ya kompyuta unapounda mipangilio, ingiza nywila. Ikiwa hujui nenosiri, wasiliana na msimamizi wako wa mfumo.

Kumbuka:
Muhimu:
  • Ili kupokea faksi kwenye kompyuta, lazima Hali ya Kupokea kwenye paneli dhibiti ya kichapishi iwekwe kwa Otomatiki. Wasiliana na msimamizi wako kwa maelezo kuhusu hali ya mipangilio ya kichapishi. Ili kuunda mipangilio kwenye paneli ya udhibiti ya kichapishi, teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Hali ya Kupokea.

  • Kompyuta iliyowekwa kupokea faksi inafaa kuwashwa kila mara. Nyaraka zilizopokewa zinahifadhiwa kwa muda kwenye kumbukumbu ya kichapishi kabla ya nyaraka zilizohifadhiwa kwenye kompyuta. Ukizima kompyuta, huenda kumbukumbu ya kichapishi ikajaa kwa kuwa haiwezi kutuma nyaraka kwenye kompyuta.

  • Idadi ya nyaraka ambazo zimehifadhiwa kwa muda katika kumbukumbu ya kichapishi huonyeshwa kwenye kwenye skrini ya nyumbani.

  • Ili kusoma faksi zilizopokewa, unahitaji kusakinisha kionyeshaji cha PDF kama vile Adobe Reader kwenye kompyuta.