Unaweza kuangalia faksi mpya na hali ya operesheni kwa kutumia ikoni ya faksi iliyoonyeshwa kwenye mwambaa wa kazi wa Windows.
Angalia ikoni.
: Kukaa ange.
: Kuangalia faksi mpya.
: Kuleta faksi mpya kumekamilika.
Bofya kulia kwenye ikoni, na kisha ubofye View Receiving Fax Record.
Skrini ya Receiving Fax Record inaonyeshwa.
Angalia tarehe na mtumaji kwenye orodha, na kisha ufungue faili iliyopokelewa kama PDF au TIFF.
Faksi zilizopokewa zinabadilishwa jina kiotomatiki kwa kutumia umbizo lifuatalo la utoaji majina.
YYYYMMDDHHMMSS_xxxxxxxxxx_nnnnn (Mwaka/Mwezi/Siku/Saa/Dakika/Sekunde_nambari ya mtumaji)
Unaweza pia kufungua kabrasha ya faksi iliyopokewa unapobofya kulia kwenye aikoni. Kwa maelezo, tazama Optional Settings kwenye FAX Utility au uangalie msaada wake (unaonyeshwa kwenye dirisha kuu).
Wakati ikoni ya faski huonyesha kuwa inakaa ange, unaweza kuangalia faksi mpya papo hapo kwa kuteua Check new faxes now.