> Kuchapisha > Kuchapisha Picha > Kuchapisha Faili za JPEG kutoka kwenye Kifaa cha Kumbukumbu > Chaguo Mahiri za Menyu kwa Mipangilio ya JPEG

Chaguo Mahiri za Menyu kwa Mipangilio ya JPEG

Kumalizia:
  • Kumalizia

    Teua Pangiliza (Mpang'o wa Ukurasa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi zilizochanganywa kwa mpangilio na kupangwa kwenye vikundi. Teua Kikundi (Kurasa Sawa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi kwa kupata kurasa zenye nambari sawa kama kikundi.

  • Toa Karatasi

    Kawaida imeteuliwa.

Ubora:

Teua Bora kwa ubora wa juu wa uchapishaji, lakini kasi ya uchapishaji inaweza kupungua.

Tatua Picha:

Teua modi hii ili kuboresha ung’avu, ulinganuzi, na ueneaji wa picha kiotomatiki. Zima uboreshaji otomatiki, teua Uboreshaji Umezimwa.

Tatua Jicho Nyekundu:

Teua Washa ili kurekebisha athari ya jicho jekundu kwenye picha kiotomatiki. Marekebisho hayatekelezwi kwenye faili asili, kwenye machapisho tu. Kulingana na aina ya picha, sehemu za picha kando na macho zinaweza kurekebishwa.

Tarehe:

Teua umbizo la tarehe ambayo picha ilipigwa au kuhifadhiwa. Tarehe haichapishwi kwa baadhi ya miundo.

Kuhifadhi Faili

Unaweza kuhifadhi data ya uchapishaji kwenye hifadhi.

  • Mpangilio:

    Chaguo iwapo utahifadhi data ya uchapishaji pekee kwenye hifadhi au la.

  • Kabrasha (Inahitajika):

    Chagua folda ambapo utahifadhi data ya uchapishaji.

  • Jina la Faili:

    Weka jina la faili.

  • Nenosiri la Faili:

    Weka nenosiri ili kuchagua faili.

  • Jina la Mtumiaji:

    Weka jina la mtumiaji.