Kusasisha Programu na Ngome

Unaweza kutatua matatizo fulani na kuboresha au kuongeza dhima kwa kusasisha programu na ngome. Hakikisha unatumia toleo lipya la programu na ngome.

Unapotumia vitendaji vifuatavyo kutoka kwenye kompyuta inayohitaji nenosiri, hakikisha unatumia mchanganyiko wa maunzi na programu ya sasa ikijumuisha kiendeshi cha kichapishi.

  • Kusajili na kutumia akaunti ya mtumijai kufikia kipengele cha kudhibiti

  • Confidential Job

  • Kufikia Hifadhi kwenye Hifadhi kutoka kwenye kompyuta

  1. Hakikisha kwamba kichapishi na kompyuta zimeunganishwa, na kompyuta imeunganishwa kwenye wavuti.

  2. Anzisha EPSON Software Updater, na usasishe programu au ngome.

    Muhimu:

    Usizime au kuchomoa kichapishi hadi kisasisho kikamilike; vinginevyo, huenda kichapishi kisifanye kazi vilivyo.

    Kumbuka:

    Ikiwa huwezi kupata programu unayotaka kusasisha katika orodha, huwezi kusasisha ukitumia EPSON Software Updater. Tafuta metoleo mapya ya programu kutoka kwa tovuti yako ya Epson.

    http://www.epson.com