> Utambazaji > Kutambaza Nakala Asili kwenye Wingu > Chaguo za Menyu za Kuchanganua kwenye Wingu

Chaguo za Menyu za Kuchanganua kwenye Wingu

Kumbuka:

Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.

Ny'i na Ny'pe/Rangi

Chagua ikiwa utatambaza kwenye monokromu au kwa rangi.

Umbizo la Faili:

Teua umbizo ambalo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.

Unapotumia PDF kama ubizo la faili, teua iwapo utahifadhi nakala zote asili kama faili moja (kurasa-nyingi) au uhifadhi kila nakala asili pekee yake (ukurasa mmoja).

Pande 2:

Tambaza pande zote za nakala asili.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

  • Ufungaji(Asili):

    Teua mwelekeo wa kuweka pamoja wa nakala asili.

Eneo la Kutambaza:

Teua eneo la kutambaza. Ili kutambaza katika eneo nzima ya glasi ya kitambazaji, teua Upeo wa Eneo.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

Aina Asili:

Teua aina ya nakala yako asili.

Mwelekeo (Asili):

Teua mwelekeo wa nakala asili.

Uzito:

Teua ulinganuzi wa taswira iliyotambazwa.

Ondoa Mand'yuma:

Teua ukolevu wa mandharinyuma. Donoa + ili kuongeza mwangaza (weupe) kwenye mandharinyuma na udonoe - ili kuikoleza (kuongeza weusi).

Iwapo utateua Otomatiki, rangi za mandharinyuma za nakala asili zimetambuliwa, na zinaondolewa au kufifishwa kiotomatiki. Haitekelezwi sahihi iwapo rangi ya mandharinyuma ni kolevu zaidi au haijatambulika.

Ondoa Kivuli:

Ondoa vivuli vya nakala asili ya ambavyo vinaonekana katika taswira iliyotambazwa.

  • Fremu:

    Ondoa vivuli katika ukingo wa nakala asili.

  • Katikati:

    Ondoa vivuli vya pambizo za kuweka pamoja vya kijitabu.

  • Ukurasa wa Nyuma:

    Weka kila eneo la upande wa nyuma unapotambaza nakala asili za pande 2.

Ondoa Mash. Panchi:

Ondoa mashimo ya panji ambayo yanaonekana kwenye taswira iliyotambazwa. Unaweza kubainisha eneo la kufuta mashimo ya panji kwa kuingiza thamani kwenye kikasha upande wa kulia.

  • Mkao wa Kufuta:

    Teua mkao ili kuondoa mashimo.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

Uta'ji Unao'a ADF:

Unaweza kuweka idadi kubwa ya nakala asili kwenye ADF katika bechi, na kuzitambaza kama kazi moja ya utambazaji.

Kuhifadhi Faili:

Unaweza kuhifadhi taswira iliyotambazwa kwenye hifadhi.

  • Mpangilio:

    Chaguo iwapo utahifadhi taswira iliyotambazwa pekee kwenye hifadhi au la.

  • Kabrasha (Inahitajika):

    Teua hifadhi ambapo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.

  • Jina la Faili:

    Weka jina la faili.

  • Nenosiri la Faili:

    Weka nenosiri ili kuchagua faili.

  • Jina la Mtumiaji:

    Weka jina la mtumiaji.