Chaguo Msingi za Menyu kwa Mipangilio ya PDF

Unaweza kuunda mipangilio ya chapisho kwa umbizo la faili za PDF kwenye kifaa chako cha kumbukumbu.

Ya hivi majuzi hadi ya zamani/Ya zamani hadi ya hivi majuzi:

Teua mpangilio wa kupanga ili kuonyesha faili kwenye skrini ya LCD.

Mipangilio ya K'si:

Bainisha mipangilio ya chanzo cha karatasi ambacho unataka kuchapisha kwacho.

Pande 2:

Teua Washa ili kuchapisha faili PDF kutumia uchapishaji wa pande 2. Pia unaweza kuteua mbinu ya kuunganisha kwenye mpangilio wa Mkao wa Ufungaji.

Agizo la Chapa:

Teua mpangilio ya uchapishaji wa kurasa anuwai wa faili PDF.

Hali ya Rangi:

Teua mpangilio wa rangi iwapo kwa kawaida unachapisha kwenye Ny'i na Ny'pe au Rangi.