Masharti ya Hifadhi/Sambaza:

Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza

Kumbuka:

Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.

Fax kichupo > Save/Forward Settings > Conditional Save/Forward

Unaweza kuweka mafikio ya kuhifadhi na/au kutuma mbele kwenye Kisanduku pokezi, vikasha vya siri, kifaa cha kumbukumbu ya nje, anwani za barua pepe, makabrasha yaliyoshirikiwa, na mashine mengine ya faksi.

Ili kubadili kati ya kuwezesha au kulemaza masharti, donoa mahali popote kwenye kipengee kilichowekwa isipokuwa kwa .

Jina:

Ingiza jina la masharti.

Hali:

Teua masharti na uweke mipangilio.

Ul'shaji wa N'ari ya Faksi ya Mtumaji

Nambari ya faksi ya mtumaji inapofanana, faksi iliyopokewa inahifadhiwa na kusambazwa.

Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO)

Anwani ndogo (SUB) zinapofanana kikamilifu, faksi iliyopokewa inahifadhiwa na kusambazwa.

Ulinganishaji kamili wa nywila

Nenosiri (SID) linafanana kikamlifu, faksi iliyopokewa inahifadhiwa na kusambazwa.

Wakati wa Kupokea

Huhifadhi na kusambaza faksi iliyopokewa wakati wa kipindi cha muda kilichobainishwa.

Hifadhi/Sambaza Mfikio:

Teua mafikio ili kuhifadhi na kutuma mbele nyaraka zilizopokewa zinazolingana na masharti. Unaweza kutumia vipengele vilivyo hapa chini kwa wakati mmoja.

Hifadhi kwenye Kasha la Faksi:

Huhifadhi faksi zilizopokelewa kwenye Kisanduku pokezi cha kichapishi au kisanduku cha siri.

Unaweza kuhifadhi hadi juimla ya nyaraka 200. Kumbuka kuwa kuhifadhi nyaraka 200 kunaweza kuwa vigumu kulingana na masharti ya matumizi kama vile ukubwa wa faili za nyaraka zilizohifadhiwa, na kutumia vipengele mbalimbali vya kuhifadhi faksi kwa wakati mmoja.

Hifadhi kwenye Kumbukumbu:

Hifadhi faksi zilizopokelewa kama faili za PDF au TIFF kwenye kifaa cha kumbukumbu ya nje kilichounganishwa kwenye kichapishi.

Hati zilizopokewa uhifadhiwa kwa muda kwenye kumbukumbu ya kichapishi kabla ya nyaraka kuhifadhiwa kwenye kifaa cha kumbukumbu kilichounganishwa kwenye kichapishi. Kwa sababu hitilafu ya kumbukumbu kujaa hulemaza kutuma na kupokea faksi, weka kifaa cha kumbukumbu kikiwa kimeunganishwa kwenye kichapishi.

Sambaza:

Husambaza faksi kwenye mashine nyingine ya faksi au huzisambaza kama faili za PDF au TIFF kwenye kabrasha iliyoshirikiwa kwenye mtandao au anwani ya barua pepe. Faksi zilizotumwa mbele hufutwa kwenye kichapishi. Kwanza ongeza mafikio ya utumaji mbele kwenye orodha ya waasiliani. Ili kusambaza kwa anwani ya barua pepe, unahitaji pia kusanidi mipangilio ya seva ya barua pepe.

  • Mfikio: Unaweza kuteua mafikio ya utumaji mbele kutoka kwenye orodha ya waasiliani uliyoiongeza mapema.

    Ikiwa umechagua kabrasha la kushiriki kwenye mtandao au anwani ya barua pepe kama mafikio wa usambazaji, tunapendekeza kwamba ujaribu kama unaweza kutuma picha iliyochanganuliwa hadi kwa mwishilio katika hali ya uchanganuzi. Teua Changanua > Barua pepe, au Changanua > Folda/FTP ya Mtandao kutoka kwenye skrini ya nyumbani, teua mafikio, na kisha anzisha utambazaji.

  • Chaguo Wakati Us'zaji Um'dikana: Unaweza kuteua iwapo utachapisha faksi iliyoshindikana au kuihifadhi kwenye Kisanduku pokezi.

Chapisha:

Huchapisha faksi zilizopokelewa.

Umbizo la Faili ya Kuhifadhi/Kusambaza:

Unaweza kuweka umbizo la faili unapohifadhi au kusambaza faksi zilizopokelewa.

Mipangiliuo ya PDF:

Kuteua PDF katika Umbizo la Faili ya Kuhifadhi/Kusambaza huwezesha mipangilio.

Nenosiri la Kufungua Hati:
Mpangilio wa Nywila:

Inawezesha kuweka nenosiri la kufungua waraka.

Nenosiri:

Weka nenosiri la kufungua waraka.

Nenosiri la Vibali:
Mpangilio wa Nywila

Huwezesha kuweka nenosiri kwa uchapishaji au uhariri wa faili ya PDF.

Nenosiri

Weka nenosiri ya idhini kwenye Nenosiri.

Uchapishaji: huruhusu uchapishaji wa faili ya PDF.

Kuhariri: huruhusu uhariri wa faili ya PDF.

Taarifa za Barua pepe:

Hutuma taarifa ya barua pepe wakati mchakato uliouteua hapa chini umekamilika. Unaweza kutumia vipengele vilivyo hapa chini kwa wakati mmoja.

Mpokeaji

Weka mafikio ya taarifa ya ukamilishaji wa mchakato.

Niarifu wakati Upokeaji umekamilika

Hutuma taarifa wakati upokeaji wa faksi umekamilika.

Niarifu wakati Uchapishaji umekamilika

Hutuma taarifa wakati uchapishaji wa faksi umekamilika.

Niarifu wakati kuh. Kif. Ku'bu kumekamilika

Hutuma taarifa wakati kuhifadhi faksi kwenye kifaa cha kumbukumbu kumekamilika.

Niarifu wakati Usambazaji umekamilika

Hutuma taarifa wakati usambazaji wa faksi umekamilika.

Ripoti ya Upitishaji:

Huchapisha ripoti ya usambazaji kiotomatiki baada ya wewe kuhifadhi au kutuma mbele faksi iliyopokewa.

Kuteua Chapisha Hitilafu Ikitokea huchapisha ripoti tu unapohifadhi au kutuma mbele faksi iliyopokewa na kosa hutokea.