Kiendeshi cha Kichapishi cha PostScript huruhusu kichapishi kupokea na kufasiri maagizo ya uchapishaji kwenye lugha ya ufafanuzi wa ukurasa iliyotumia kutoka kwenye kompyuta na kuchapisha ipasavyo. Hii ni mwafaka katika kuchapisha kutoka kwenye programu zinatozingatia PostScript zinazotumika kwa DTP.
Ili uweke mipangilio inayotumika kwenye programu unayotumia peke yake, ifikie kutoka kwa programu hiyo.
Chagua Chapisha au Usanidi wa Uchapishaji katika menyu ya Faili. Chagua printa yako, na kisha ubofye Mapendeleo au Sifa.
Utendaji hutofautiana kulingana na programu. Angalia msaada wa programu kwa maelezo.
Kuweka mipangilio inayotumika kwenye programu zote, ifikie kutoka kwa paneli dhibiti.
Windows 10/Windows Server 2019/Windows Server 2016
Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Mfumo wa Windows > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi kwenye Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uteue Mapendeleo ya uchapishaji
Windows 8.1/Windows 8/Windows Server 2012 R2/Windows Server 2012
Teua Eneo Kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uteue Mapendeleo ya uchapishaji
Windows 7/Windows Server 2008 R2
Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.
Windows Vista/Windows Server 2008
Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Kichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.
Windows XP/Windows Server 2003 R2/Windows Server 2003
Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Vichapishi na Maunzi Nyingine > Vichapishi na Faksi. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.
Ikoni ya printa iliyo kwenye mwambaa kazi wa eneo kazi ni ikoni ya mkato ya kukuwezesha ufikie kiendeshi cha printa kwa urahisi.
Ukibofya ikoni ya printa na uchague Mipangilio ya Printa, unaweza kufikia dirisha sawa la mipangilio ya printa na linaloonekana katika paneli dhibiti. Ukibofya ikoni hii mara mbili, unaweza kuona hali ya printa.