> Kutatua Matatizo > Kutatua Tatizo > Angalia muunganisho wa kichapishi.

Angalia muunganisho wa kichapishi.

Angalia iwapo kuna tatizo na muunganisho wa kichapishi.

Eneo la ukaguzi

Suluhisho

Je, kichapishi kimeunganishwa kwenye mtandao vizuri?

Endesha ukaguzi wa muunganisho wa mtandao ili kuangalia muunganisho wa mtadao.

Kwenye skrini ya LCD, teua > Jinsi ya... > Wakati huwezi kuunganisha kwenye mtandao. Chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao, na kisha uulize msimamizi kutatua shida iwapo kuna shida ya muunganisho.

Je, kiendeshi cha kichapishi kimesakinishwa kwenye kompyuta yako?

Unaweza kuangalia iwapo kiendeshi cha kichapishi kimesakinishwa kwa kuangalia Mipangilio > Vifaa > Vichapishi kwenye kompyuta yako. Tazama taarifa inayohusiana na maelezo.

Je, maelezo ya kichapishi yameonyeshwa kwenye kompyuta yako?

Unaweza kutumia Kifuatiliaji cha Hali ya Epson 3 ili kuangalia hali ya muunganisho kati ya kompyuta na kichapishi. Tazama taarifa inayohusiana na maelezo.

Ikiwa huwezi kuangalia hali ya kichapishi, kituo sahihi huenda hakijateuliwa. Ukiunganisha kwenye kichapishi katika mtandao, tunapendekeza uteue EpsonNet Print Port. Iwapo EpsonNet Print Port haipatikani, sakinisha tena kiendeshi cha kichapishi.

Je, muunganisho wa pasiwaya wa LAN (Wi-Fi) umetatizwa au hauwezi kuunganisha wakati ambapo unatumia kifaa cha USB 3.0 kwenye kompyuta yako?

Unapounganisha kifaa kwenye kituo tayarishi cha USB 3.0 kwenye Mac, ukatizaji wa mawimbi ya redio unaweza kutokea. Jaribu yafuatayo.

  • Weka kifaa kilichounganishwa kwenye kituo tayarishi cha USB 3.0 mbali na kompyuta.

  • Zima vifaa vyovyote vya USB 3.0 ambavyo havitumiki au viunganishe tu panapohitajika.

  • Unganisha kwenye SSID kwa masafa ya 5 GHz.

Je, kompyuta yako au kifaa chako mahiri kinaweza kuunganishwa kwenye mtandao?

Angalia iwapo unaweza kutazama tovuti kwenye kompyuta yako au kifaa mahiri (mawasiliano ya data yamezimwa). Iwapo huwezi kuitazama, kuna tatizo na mtandao. Mwulize msimamizi kutatua shida.