Haiwezi kuunganishwa kwenye Mtandao

Huenda tatizo likawa mojawapo ya yafuatayo.

Tatizo fulani limetokea kwenye kifaa cha mtandao kwa muunganisho wa Wi-Fi.

Suluhisho

Zima vifaa unavyotaka kuunganisha kwenye mtandao. Subiri karibu sekunde 10, na kisha uwashe vifaa katika mpangilio ufuatao; kipanga njia pasiwaya, kompyuta au kifaa maizi, na kisha kichapishi. Sogeza kichapishi na kompyuta au kifaa mahiri karibu na kipanga njia pasiwaya ili kusaidia na mawasiliano ya mawimbi ya redio, na kisha jaribu kutengeneza mipangilio ya mtandao tena.

Vifaa haviwezi kupokea mawimbi kutoka kwenye kipanga njia pasiwaya kwa sababu vimetenganishwa kwa mbali sana.

Suluhisho

Baada ya kusogeza kompyuta au kifaa maizi na kichapishi karibu na kipanga njia pasiwaya, zima kipanga njia pasiwaya kisha ukiwashe tena.

Unapobadilisha kipanga njia pasiwaya, mipangilio hailingani na kipanga njia kipya.

Suluhisho

Weka mipangilio ya muunganisho tena ili ilingane na kipanga njia pasiwaya kipya.

SSID zilizounganishwa kutoka kompyuta au kifaa maizi na komyuta ni tofauti.

Suluhisho

Unapotumia vipanga njia pasiwaya vingi kwa wakati mmoja au kipanga njia pasiwaya kina SSID nyingi na vifaa vimeunganishwa kwenye SSID tofauti, huwezi kuunganisha kipanga njia pasiwaya.

Unganisha kompyuta au kifaa maizi kwenye SSID moja kama kichapishi.

Kitenganishi cha faragha kwenye kipanga njia pasiwaya kinapatikana.

Suluhisho

Vipanga njia unuwai vingi vina kipengele cha kitenganishi cha faragha kinachozuia mawasiliano kati ya vifaa vilivyounganishwa. Iwapo huwezi kuwasiliana kati ya kichapishi na kompyuta au kifaa maizi hata iwapo vimeunganishwa kwenye mtandao mmoja, lemaza kitenganishi cha faragha kwenye kipanga njia pasiwaya. Tazama mwongozo uliotolewa ulio na kipanga njia pasiwaya kwa maelezo.

Anwani ya IP haijapangiwa ipasavyo.

Suluhisho

Iwapo anwani ya IP iliyopangiwa kichapishi ni 169.254.XXX.XXX, na barakoa ndogo ni 255.255.0.0, huenda anwani ya IP isipangiwe kwa usahihi.

Teua Settings > Network Settings > Advanced kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, kisha uangalie anwani ya IP na barakoa ndogo iliyopangiwa kichapishi.

Washa upya kipanga njia chako pasiwaya au weka upya mipangilio ya mtandao kwa kichapishi.

Kuna tatizo na mipangilio ya mtandao kwenye kompyuta hii.

Suluhisho

Jaribu kufikia tovuti yoyote kutoka kwenye kompyuta yako ili kuhakikisha kuwa mipangilio ya mtandao wa kompyuta yako ni sahihi. Iwapo huwezi kufikia tovuti yoyote, kuna tatizo kwenye kompyuta.

Angalia muunganisho wa mtandao wa kompyuta. Tazama hati iliyotolewa yenye kompyuta kwa maelezo.

Kifaa kilichounganishwa kwenye kituo cha USB 3.0 kinasababisha mtafaruku wa mawimbi.

Suluhisho

Unapounganisha kifaa kwenye kituo tayarishi cha USB 3.0 kwenye Mac, ukatizaji wa mawimbi ya redio unaweza kutokea. Jaribu yafuatayo iwapo huwezi kunganisha kwenye LAN pasiwaya (Wi-Fi) au iwapo operesheni hazitakuwa thabiti.

  • Weka kifaa kilichounganishwa kwenye kituo tayarishi cha USB 3.0 mbali na kompyuta.

  • Unganisha kwenye SSID kwa masafa ya 5 GHz.

Angalia yafuatayo ili kkunganisha kichapsihi kwenye SSID.

Kichapishi kimeunganishwa kwa Ethaneti kwa kutumia vifaa vinavyotumia IEEE 802.3az (Ethaneti Inayotunza Nishati).

Suluhisho

Unapounganisha kichapishi kwa Ethaneti ukitumia kifaa kinachotumia IEEE 802.3az (Energy Efficient Ethernet), matatizo yafuatayo yanaweza kutokea kwa kutegemea kitovu au kipanga njia unachotumia.

  • Muunganisho unakuwa dhaifu, kichapishi kimeunganishwa na kutenganishwa tena na tena.

  • Haiwezi kuunganisha kwenye kichapishi.

  • Kasi ya mawasiliano inajikokota.

Fuata maelekezo hapa chini ili kulemaza IEEE 802.3az kwa kichapishi kisha uunganishe.

  1. Ondoa kebo ya Ethaneti iliyounganishwa kwenye kompyuta na kichapishi.

  2. Ikiwa IEEE 802.3az ya kompyuta imewezeshwa, ilemaze.

    Tazama hati iliyotolewa yenye kompyuta kwa maelezo.

  3. Unganisha kompyuta na kichapishi ukitumia kebo ya Ethaneti moja kwa moja.

  4. Kwenye kichapishi, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao.

    Kuchapisha Ripoti ya Muunganisho wa Mtandao

  5. Angalia anwani ya IP ya kichapishi kwenye ripoti ya muunganisho wa mtandao.

  6. Kwenye kompyuta, fikia Web Config.

    Zindua kivinjari Wavuti, na kisha uingize anwani ya IP ya kichapishi.

    Kuendesha Usanidi wa Wavuti kwenye Kivinjari cha Wavuti

  7. Teua Advanced Settings kutoka kwenye orodha upande wa juu kulia wa dirisha.

  8. Teua Network Settings > Wired LAN.

  9. Teua OFF kwa IEEE 802.3az.

  10. Bofya Next.

  11. Bofya OK.

  12. Ondoa kebo ya Ethaneti iliyounganishwa kwenye kompyuta na kichapishi.

  13. Ikiwa ulilemaza IEEE 802.3az ya kompyuta katika hatua ya 2, iwezeshe.

  14. Unganisha kebo za Ethaneti ulizoondoa kwenye hatua ya 1 kwenye kompyuta na kichapishi.

Iwapo bado tatizo linatokea, vifaa kando na kichapishi vinaweza kuwa vinatumia tatizo.