Pakia karatasi ya ukubwa wa A4 kwenye kichapishi.
Teua Maintenance kwenye skrini ya nyumbani.
Teua Power Cleaning.
Usafishaji unapokamilika, chapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli tena. Angalia kwamba mistari yote kwenye ruwaza ya kuangalia nozeli imechapishwa ipasavyo.
Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kuendesha Power Cleaning, subiri kwa angalau saa 6 bila kuchapisha kisha uchapishe ruwaza ya uangaliaji nozeli tena. Endesha Cleaning au Power Cleaning tena kwa kutegemea ruwaza iliyochapishwa. Ikiwa ubora bado hajuaimarika, wasiliana na timu ya usaidizi ya Epson.