Kwa kutegemea viwango vya wino, unaweza kuendelea kuchapisha kwa muda bila kubadilisha vibweta vya wino.
Endelea Kuchapisha kwa Muda ukitumia Wino Mweusi Pekee
Endelea Kuchapisha ili Kuhifadhi Wino Mweusi (kwa Windows Pekee)
Iwapo trei ya CD/DVD imechomekwa, ondoa trei.
Fanya moja kati ya zifuatazo.
Ondoa vibweta vipya vya wino kutoka kwenye kifurushi chake, na kisha udonoe Next.

Hakikisha kifuniko kinaangalia juu, na kisha ukiondoe.

Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye picha. Kufanya hivyo kunaweza kuzuia utendaji na uchapishaji wa kawaida.

Fungua kitengo cha kitambazaji wakati jalada la waraka limefungwa.
Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazaji. La sivyo unaweza kujeruhiwa.

Thibitisha ujumbe, na kisha udonoe Start.
Kishikio cha kibweta cha wino husonga katika nafasi ya ubadilishaji. Hata hivyo, kishikilio cha kibweta cha wino kinaweza kurudi baada ya dakika kadha. Katika hali kama hiyo, rudia hatua ya 2 hadi ya 6.
Unapobadilisha katriji za wino, zibadilishe kwa mkao sahihi wa ubadilishaji. Iwapo utabadilisha hizi kwenye mkao mbaya, kosa la utambuiz linatokea. Iwapo kosa litatokea, chomeka tena hii kwa mkao sahihi wa ubadilishaji.

Sukuma kichupo ili kufungua kishikilio cha kibweta cha wino, na kisha uondoe kibweta kimshazari.
Badilisha vibweta vya wino moja baada ya kingine haraka iwezekanavyo. Iwapo utabadilisha vibweta viwili au zaidi kwa wakati mmoja au iwapo ubadilishaji unachukua muda, baadhi ya wino unaweza kutumika kushughulikia utendakazi wa kichapishi.

Chomeka kibweta cha wino kimshazari kwenye kishikilio cha kibweta na ukisukume chini taratibu hadi kitoe sauti katika eneo.

Funga kitengo cha kitambazaji, na kisha udonoe Completed.
Fuata maagizo ya kwenye skrini.
Ukiondoa katriji kutoka kwa printa kwa matumizi ya baadaye au kuitumpa, hakikisha umefunika lango la kutoa wino la katriji ili kuzuia wino kukauka au kuzuia maeneo yaliyo kando yasimwagikiwe na wino. Weka kifuniko salama hadi kifike sehemu inayostahili.

Baada ya kufunga kariji ya wino, taa ya nisha inaendelea kumweka wakati printa inanyonya wino. Usizime printa wakati wa kunyonya wino. Ikiwa unyonyaji wa wino haujakamilika, huwezi kuchapisha.
Usichomeke trei ya CD/DVD hadi kuongeza wino kukamilike.