> Kunakili > Kunakili Nakala Asili

Kunakili Nakala Asili

Sehemu hii inafafanua jinsi ya kutumia menyu ya Nakili kwenye paneli dhibiti ili kunakili nakala asili.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kuweka Karatasi

  2. Weka nakala za kwanza.

    Kuweka Nakala Asili

  3. Teua Nakili kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua kichupo cha Nakili, na kisha uteue Nyeusi na Nyeupe au Rangi.

  5. Weka idadi ya nakala.

  6. Donoa .

    Kumbuka:
    • Iwapo utateua Hakiki, unaweza kuangalia taswira zilizotambazwa.

    • Rangi, ukubwa, na ukingo wa taswira iliyonakiliwa ni tofauti kiasi kutoka kwenye nakala asili.