Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.
Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.
Kichupo cha Fax > Basic Settings
Iwapo ingizo la nywila limeonyeshwa, ingiza nywila.
Teua kazi ya utumaji wa faksi. Tunapendekeza uchague Polepole(9,600bps) wakati hitilafu ya mawasiliano hutokea mara kwa mara, wakati wa kutuma/kutuma faksi ng'ambo, au wakati unatumia huduma ya simu ya IP (VoIP).
Husahihisha hitilafu kiotomatiki katika utumaji wa faksi (Modi ya Usahihishaji wa Hitilafu), ambazo mara nyingi husababishwa na kelele ya laini ya simu. Ikiwa hii imelemazwa, huwezi kutuma au kupokea hati za rango.
Hutambua toni ya kudayo kabla ya kuanza kudayo. Ikiwa printa imeunganishwa kwenye PBX (Ubadilishanaji Binafsi wa Tawi) au laini dijitali ya simu, huenda printa ishindwe kuanza kudayo. Katika haki hii, badilisha mpangilio wa Aina ya Laini kuwa wa PBX. Ikiwa hii haitfanya kazi, lemaza kipengele hiki. Hata hivyo, kulemaza kipengele hiki kunaweza kufuta tarakimu ya kwanza ya nambari ya faksi na itume faksi kwa nambari isiyo sahihi.
Teua aina ya mfumo wa simu ambao umeunganisha printa. Wakati imewekwa kuwa Pigo, unaweza kubadilisha modi ya kudayo kwa muda kutoka papo na kuwa toni kwa kubonyeza
(“T” inaingizwa) wakati unaingiza nambari kwenye skrini ya juu ya faksi. Mpangilio huu huenda usipatikane kulingana na eneo au nchi yako.
Chagua aina ya laini uliyounganisha printa.
Wakati unatumia kichapishi katika mazingira ambayo yanatumia virefusho na yanahitaji msimbo wa ufikiaji wa nje, kama vile 0 na 9, ili upate mstari wa nje, teua PBX. Kwa mazingira ambayo yanatumia modemu ya DSL au adapta ya temino, unapendekezwa pia uweke kwa PBX.
Teua Tumia, na kisha sajili mdsimbo wa ufikiaji wa nje kama vile 0 au 9. Kisha, unapotuma faksi kwa nambari ya faksi ya nje, weka # (hashi) badala ya msimbo halisi wa kufikia. # (hashi) inafaa kutumika kwenye Waasiliani kama msimbo wa ufikiaji wa nje. Iwapo msimbo wa ufikiaji wa nje kama vile 0 au 9 imewekwa katika mwasiliani, huwezi kutuma faksi kwa mwasiliani. Katika hali hii, weka Msimbo wa Ufikiaji hadi Usitumie, vinginevyo unafaa kubadilisha msimbo kwenye Waasiliani hadi #.
Ingiza jina lako la mtumaji na nambari ya faksi. Hizi huonekana kama kichwa kwenye faksi zinazotoka.
Nambari Yako ya Simu: Unaweza kuingiza hadi vibambo 20 kwa kutumia 0–9 + au nafasi. Kwa Web Config, unaweza kuhifadhi hadi nyaraka 30.
Kijajuu cha Faksi: Unaweza kusajili hadi majina 21 ya watumaji inavyohitajika. Unaweza kuingiza hadi vibambo 40 kwa kila jina la mtumaji. Kwa Web Config, ingiza kijajuu kwenye Msimbosare (UTF-8).
Ikiwa umejisajili kwa huduma ya mzunguko tofauti kutoka kwa kampuni yako ya simu, chagua ruwaza ya mzunguko ya kutumiwa kwa faksi zinazoingia. Huduma tofauti ya mzunguko, inayotolewa na makampuni mengi ya simu (jina la huduma hutofautiana na kampuni), hukuwezesha kuwa na nambari kadhaa za simu kwenye laini moja ya simu. Kila nambari inapewa ruwaza tofauti ya mzunguko. Unaweza kutumia nambari moja kwa simu za sauti na nyingine kwa simu za faksi. Kulingana na eneo, mpangilio huu huenda Washa au Zima.
Teua idadi ya mizunguko inayofaa kufanyika kabla ya printa kupokea faksi kiotomatiki.
Unapojibu simu ya faksi inayoingia kupitia simu iliyounganishwa kwenye kichapishi, unaweza kuanza kupokea faksi kwa kuingiza msimbo ukitumia simu.
Weka msimbo wa kuanza wa Pokea kwa Mbali. Ingiza vibambo viwili kwa kutumia 0–9, *, #.
Teua chaguo za kukataa faksi za barua taka.
Orodha ya Nambari Zilizozuiwa: Iwapo nambari ya simu ya mhusika mwingine ipo kwenye orodha ya idadi iliyokataliwa, weka iwapo utakataa faksi zinazoingia.
Kijajuu cha Faksi kiko Tupu: Iwapo nambari ya si mu ya mhusika mwingine imezuiwa, weka iwapo utakataa kupokea faksi.
Mp. simu hay. ktk W'ni: Iwapo nambari ya simu ya mhusika mwingine haipo kwenye waasiliani, weka iwapo utakataa kupokea faksi.
Unaweza kusajili hadi nambari 30 za faksi ili kukataa faksi na simu. Ingiza hadi vibambo 20 kwa kutumia 0–9, *, #, au nafasi.