Unaweza kubainisha wapokeaji kwenye kichupo cha Mpokeaji ili kutuma faksi kwa kutumia mbinu zifuatazo.
Teua Ingiza Moja kwa Moja, ingiza nambari ya faksi kwenye skrini inayoonyeshwa, na kisha udonoe Sawa.
- Ili kuongeza kusitisha (sitisha kwa sekunde tatu wakati wa kupiga) ingiza kistari kifupi (-).
- Ikiwa utaweka msimbo wa ufikiaji wa nje katika Aina ya Laini, ingiza “#” (hashi) badala ya msimbo wa ufikiaji wa nje mwanzoni wa nambari ya faksi.
Iwapo huwezi kuingiza nambari ya faksi kikuli, Vikwazo vya Kupiga Moja kwa moja kwenye Mipangilio ya Usalama imewekwa kwa Washa. Teua wapokeaji wa faksi kutoka kwenye orodha ya waasiliani au historia ya faksi iliyotumwa.
Teua Waasiliani na uteue wapokeaji unaotaka kutuma. Ikoni ifuatayo inaonyesha orodha ya waasiliani.

Ili kutafuta mpokeaji kutoka kwenye orodha ya waasiliani, teua
.
Iwapo mpokeaji unayetaka kumtumia bado hajasajiliwa kwenye Waasiliani, teua
ili kumsajili.
Teua
(Hivi karibuni), kisha uteue mpokeaji.
Teua mpokeaji aliyesajiliwa kama Assign to Frequent Use katika Web Config.
Ili kufuta wapokeaji uliowaingiza, onyesha orodha ya wapokeaji kwa kudonoa sehemu kwenye skrini ambayo inaonyesha nambari ya faksi au iidadi ya wapokeaji kwenye skrini ya LCD, teua mpokeaji kutoka kwenye orodha, na kisha uteue Ondoa.