/ Kutuma Faksi / Kutuma Faksi kwa Kutumia Kichapishi / Kutuma Faksi kwa Kutumia Paneli ya Udhibiti / Kudayo Kutuma Faksi kutoka kwa Huduma ya Simu ya Nje

Kudayo Kutuma Faksi kutoka kwa Huduma ya Simu ya Nje

Unaweza kutuma faksi kwa kudayo ukitumia simu iliyounganishwa unapotaka kuzungumza kwenye simu kabla ya kutuma faksi, au wakati mashine ya faksi ya mpokeaji haibadilishi kwa faksi kiotomatiki.

  1. Weka nakala za kwanza.

    Unaweza kutuma hadi kurasa 100 katika utumaji huu.

  2. Inua mkono wa kifaa cha simu na kisha udayo nambari ya faksi ya mpokeaji kwa kutumia simu.

    Kumbuka:

    Mpokeaji anapojibu simu, unaweza kuzungumza na mpokeaji.

  3. Teua Faksi kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  4. Bonyeza kitufe cha Sawa, na kisha uteue Mipangi. Utambazaji au Mipan. Kutuma Faksi na kisha uweke mipangilio kama vile mwonekano na mbinu ya utumaji inavyohitajika.

  5. Unaposikia toni ya faksi, bonyeza kitufe cha , na kisha ukate simu.

    Kumbuka:

    Wakati nambari inapigwa kupitia simu iliyounganishwa, huwa inachukua muda mrefu kutuma faksi kwa sababu kichapishi hufanya utambazaji na utumaji wakati mmoja. Wakati unatuma faksi, huwezi kutumia vipengele vingine.

  6. Wakati utumaji umekamilika, ondoa nakala asili.