/ Utambazaji / Utambazaji Kupitia Paneli Dhibiti / Utambazaji kwa Kompyuta

Utambazaji kwa Kompyuta

Kumbuka:

Baada ya kutambaza, sakinisha Epson Scan 2 na Epson Event Manager kwenye kompyuta yako.

  1. Weka nakala za kwanza.

  2. Teua Changanua kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  3. Teua jinsi ya kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kompyuta kutoka kwenye menyu zifuatazo, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

    • Kwenye Kompyuta (JPEG): Uhifadhi picha iliyotambazwa katika umbizo la JPEG.
    • Kwenye Kompyuta (PDF): Uhifadhi picha iliyotambazwa katika umbizo la PDF.
    • Kwenye Kompyuta (Barua pepe): Huanzisha huduma ya barua pepe kwenye kompyuta, na kisha huiambatisha kiotomatiki kwenye barua pepe.
    • Kwenye Kompyuta (Maalum): Huhifadhi picha iliyotambazwa kwa kutumia mipangilio kwenye Epson Event Manager. Unaweza kubadilisha mipangilio ya utambazaji kama vile ukubwa wa kutambaza, kabrasha la kuhifadhi, au umbizo la kuhifadhi.
  4. Teua kompyuta unayotaka kuhifadhi picha zilizotambazwa.

    Kumbuka:
    • Unaweza kubadilisha mipangilio ya utambazaji kama vile ukubwa wa kutambaza, kabrasha la kuhifadhi, au umbizo la kuhifadhi, kwa kutumia Epson Event Manager.

    • Wakati kichapishi kimeunganishwa kwenye mtandao, unaweza kuteua kompyuta ipi ambayo unataka kuhifadhi taswira iliyotambazwa. Unaweza kuonyesha hadi kompyuta 20 kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Iwapo utaweka Network Scan Name (Alphanumeric) kwenye Epson Event Manager, inaonyeshwa katika paneli dhibiti.

  5. Bonyeza kitufe cha .