/ Mipangilio ya Faksi / Kutayarisha kichapishi Kutuma na Kupokea Faksi (Kwa Kutumia Kis. Mpang. Faksi)

Kutayarisha kichapishi Kutuma na Kupokea Faksi (Kwa Kutumia Kis. Mpang. Faksi)

Kis. Mpang. Faksi inasanidi vipengele msingi vya faksi ili kufanya kichapishi kuwa tayari kutumia na kupokea faksi.

Sogora huonyeshwa kiotomatiki wakati kichapishi kimewashwa kwa mara ya kwanza. Pia unaweza kuonyesha sogora wewe mwenyewe kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Unahitaji kuendesha sogora tena ikiwa sogora itarukwa wakati kichapishi kimewashwa kwa mara ya kwanza au wakati mazingira ya muunganisho yamebadilika.

  • Vipengele vilivyo hapa chini ndivyo vinawekwa kupitia sogora.

    • Kijajuu (Nambari Yako ya Simu na Kijajuu cha Faksi)

    • Hali ya Kupokea (Otomatiki au Mwenyewe)

  • Vipengele vilivyo hapa chini vinawekwa kiotomatiki kulingana na mazingira ya muunganisho.

    • Hali ya Kupiga simu (kama vile Toni au Pigo)

    • Aina ya Laini (PSTN au PBX)

    • Ug'ji Mli. kup. Simu

    • Mpangilio wa DRD

  • Vipengele vingine katika Mipangilio Msingi vinasalia vilivyo.

Washa Kis. Mpang. Faksi ili ufanye Mipangilio Msingi, ukifuata maelekezo yaliyo kwenye skrini.

  1. Hakikisha kichapishi kimeunganishwa kwenye laini ya simu.

    Kumbuka:

    Kwa sababu ukaguzi wa muunganisho otomatiki wa faksi hufanywa mwisho wa sogora, lazima kichapishi kiunganishwe kwenye laini ya simu kabla ya kuanzisha sogora.

  2. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  3. Teua Mipangilio ya Faksi > Kis. Mpang. Faksi.

  4. Angalia ujumbe ulioonyeshwa kwenye skrini, na kisha uteue Endelea.

    Sogora inaanza.

  5. Kwenye skrini ya kuingiza kichwa cha faksi, ingiza jina la mtumaji kama vile jina la kampuni yako, na kisha uteue OK.

    Kumbuka:

    Jina lako la mtumaji na nambari yako ya faksi inaonekana kama kichwa kwenye faksi inayotoka.

  6. Kwenye skrini ya kuingiza nambari ya simu, ingiza nambari yako ya faksi, na kisha uteue Endelea

  7. Kwenye skrini ya Mpangilio wa DRD, weka mipangilio ifuatayo.

    • Ikiwa umejisajili kwa huduma ya mlio tofauti kutoka kwa kampuni yako ya simu: Teua Mipangilio, na kisha uteue ruwaza ya mlio ya kutumiwa kwa faksi zinazoingia.
      - Iwapo utateua Zote, nenda kwenye hatua ya 8.
      - Iwapo utateue mpangilio wowote mwingine, Hali ya Kupokea imewekwa otomatiki kwa Otomatiki. Nenda kwenye hatua ya 10.
    • Iwapo huhitaji kuweka chaguo hili: Teua Ruka, na kisha uende kwenye hatua ya 8.
    Kumbuka:
    • Huduma tofauti za mzunguko, zinazotolewa na makampuni mengi ya simu (jina la huduma hutofautiana na kampuni), hukuwezesha kuwa na nambari kadhaa za simu kwenye laini moja ya simu. Kila nambari inapewa ruwaza tifauti ya mzunguko. Unaweza kutumia nambari moja kwa simu za sauti na nyingine kwa simu za faksi. Chagua ruwaza ya mzunguo iliyopewa kwa simu za faksi katika DRD.

    • Kulingana na eneo, Washa na Zima huonekana kama chaguo za DRD. Chagua Washa ili utumie kipengele tofatui cha mzunguko.

  8. Kwenye skrini ya Mpang. Modi ya Kupokea, chagua kama unatumia kifaa chako cha simu kilichounganishwa kwenye printa.

    • Wakati umeunganishwa: Teua Ndiyo, na uende kwenye hatua inayofuata.
    • Wakati haijaunganishwa: Teua La na uende kwenye hatua ya 10. Hali ya Kupokea imewekwa kwenye Otomatiki.
  9. Kwenye skrini ya Mpang. Modi ya Kupokea, chagua kama unataka kupokea faksi kiotomatiki.

    • Ili upokee kiotomatiki: Teua Ndiyo. Hali ya Kupokea imewekwa kwenye Otomatiki.
    • Ili upokee kikuli: Teua La. Hali ya Kupokea imewekwa kwenye Mwenyewe.
  10. Angalia ujumbe ulioonyeshwa kwenye skrini ya uthibitisho, na kisha uteue Endelea.

    Ili usahihishe au kubadilisha mipangilio, bonyeza kitufe cha .

  11. Kwenye skrini ya Angalia Muunganisho wa Faksi, teua Anza Kukagua ili utekeleze ukaguzi wa muunganisho wa faksi, na wakati skrini inakuambia uchapishe matokeo ya ukaguzi, teua Chapisha.

    Ripoti ya matokeo ya ukaguzi inayoonyesha hali ya muunganisha imechapishwa.

    Kumbuka:
    • Ikiwa kuna hitilafu zozote ambazo zimeripotiwa, fuata maelekezo yaliyo kwenye ripoti ili uzitatue.

    • Ikiwa skrini ya Chagua Aina ya Laini imeonyeshwa, chagua aina ya laini.

      - Wakati unaunganisha kichapishi kwenye mfumo wa simu wa PBX au adapta ya taminali, teua PBX.

      - Wakati unaunganisha kichapishi kwenye laini wastani ya simu, teua PSTN. Wakati ujumbe wa kulemaza utambuzi wa toni ya kupiga unaonyeshwa kwenye skrini, bonyeza kitufe cha OK. Hata hivyo, kulemaza utambuzi wa toni kunaweza kusababisha kichapishi kiruke tarakimu ya kwanza ya nambari ya faksi wakati wa kudayo na itume faksi kwa nambari isiyo sahihi.