/ Kutayarisha Kichapishi / Kuweka Nakala Asili / Kuweka Nakala Asili kwenye Glasi ya Kichanganuzi

Kuweka Nakala Asili kwenye Glasi ya Kichanganuzi

Tahadhari:

Chunga usijibane mkono au vidole wakati unafungua au kufunga kifuniko cha hati. La sivyo unaweza kujeruhiwa.

Muhimu:

Wakati unaweka nakala nyingi za kwanza kama vile vitabu, zuia mwangaza kutoka nje kumulika kwenye glasi ya kichanganuzi moja kwa moja.

  1. Fungua kifuniko cha hati.

  2. Ondoa vumbi au madoadoa yoyote kwenye eneo la glasi ya kichanganuzi kwa kutumia kitambaa laini na safi.

    Kumbuka:

    Iwapo kuna taka au uchafu wowote kwenye glasi ya kichanganuzi, kiwango cha utambazaji kinaweza kupanuka ili kuujumuisha, kwa hivyo taswira ya nakala asili inaweza kuwekwa visivyo au kupunguzwa.

  3. Weka nakala ya kwanza ikiangalia chini na uitelezeshe hadi kwa alama ya kona.

    Kumbuka:
    • Masafa ya 1.5 mm kutoka kwa kona ya glasi ya kichanganuzi hayachapishwi.

    • Wakati nakala ya kwanza imewekwa katika ADF na kwenye glasi ya kichanganuzi, kipaumbele hupewa nakala za kwanza zilizo ndani ya ADF.

  4. Funga kifuniko polepole.

    Muhimu:

    Usitumie nguvu mingi zaidi kwenye glasi ya kichanganuzi au jalada la waraka. Vinginevyo, huenda zikaharibika.

  5. Ondoa nakala za kwanza baada ya kutambaza.

    Kumbuka:

    Ukiwacha nakala za kwanza kwenye glasi ya kichanganuzi kwa muda mrefu, zinaweza kukwama kwenye kioo.