/ Kutatua Matatizo / Matatizo ya Uchapishaji / Picha Zinachapishwa katika Rangi Zisizotarajiwa

Picha Zinachapishwa katika Rangi Zisizotarajiwa

Unapochapisha kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi cha Windows, mpangilio wa urekebishaji picha kiotomatiki wa Epson unatekelezwa kwa chaguo-msingi kulingana na aina ya karatasi. Jaribu kubadilisha mpangilio.

Kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi, teua Kaida kwenye Usahihishaji wa Rangi, na kisha ubofye Iliyoboreshwa. Badilisha mpangilio wa Usahihishaji wa Eneo kutoka Ur'aji Oto'ki hadi chaguo jingine lolote. Iwapo kubadilisha mpangilio hakufanyi kazi, tumia mbinu yoyote ya marekebisho ya rangi kando na Ubora Picha kwenye Usimamiaji wa Rangi.