Ukitumia Hali ya Picha kwenye Epson Scan 2, unaweza kutambaza nakala asili kwa vipengele mbalimbali vya marekebisho ya taswira ambayo ni muhimu kwa picha.
Weka nakala za kwanza.
Kwa kuweka nakala nyingi asili kwenye kioo cha kitambazaji, unaweza kuzitambaza zote kwa wakati mmoja.Hakikisha kuna nafasi wa angalau 20 mm kati ya nakala asili.
Anzisha Epson Scan 2.
Teua Hali ya Picha kutoka kwa orodha ya Hali.
Weka mipangilio ifuatayo kwenye kichupo cha Mipangilio Kuu.

Mpangilio wa Chanzo cha Hati umerekebishwa kama Glasi ya Kichanganuzi, na mpangilio Aina ya Hati unarekebishwa kama Inayoangaza.(Inayoangaza humaanisha nakala asili ambazo sio wazi, kwa mfano karatasi au picha za kawaida.)Huwezi kubadilisha mipangilio hii.
Bofya Hakiki.
Dirisha la uhakiki hufunguka, na taswira zilizohakikiwa zinaonyeshwa kama vijipicha.

Ili kuhakiki eneo kamili lililotambazwa, futa kisanduku cha kuteua cha Kijipicha kutoka upande wa juu wa dirisha la uhakiki.
Thibitisha uhakiki, na ufanye mipangilio ya marekebisho kwenye kichupo cha Mipangilio ya hali ya Juu ikiwezekana.

Unaweza kurekebisha taswira iliyotambazwa kwa kutumia mipangilio ya kina ambayo ni muhimu kwa picha, kama ifuatayo.
Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Kulingana na nakala asili, huenda taswira iliyotambazwa isirekebishwe sahihi.
Wakati vijipicha vingi vimeundwa, unaweza kurekebisha ubora wa taswira kwa kila kijipicha.Kulingana na vipengee vya urekebishaji, unaweza kurekebisha ubora wa taswira zilizotambazwa pamoja kwa kuteua vijipicha vingi.
Weka mipangilio ya kuhifadhi faili.

Bofya Changanua.