/ Kuweka Karatasi / Kuweka Karatasi Katika Eneo la Nyuma la Karatasi

Kuweka Karatasi Katika Eneo la Nyuma la Karatasi

  1. Fungua kilinda sehemu ya kuingiza karatasi, panua kishikilia karatasi, na kisha ukiinamishe nyuma.

  2. Telezesha mwongozo wa kingo kushoto.

  3. Weka karatasi wima upande wa kulia wa eneo la nyuma la karatasi upande unaweza kuchapishwa ukiangalia juu.

    Muhimu:

    Usiweke zaidi ya upeo wa idadi ya karatasi uliotajwa kwa karatasi. Kwa karatasi tupu, usiweke zaidi ya mstari unaoonyeshwa na alama ya pembetatu kwenye mwongozo wa kingo.

    • Bahasha
    • Karatasi iliyotobolewa kabla
    Kumbuka:
    • Weka karatasi moja bila mashimo ya kubana kutoka juu au chini.

    • Rekebisha mkao wa uchapishaji wa faili yako ili uepuke kuchapisha juu ya mashino hayo.

  4. Telezesha mwongozo wa kingo kwenye ukingo wa karatasi, na kisha ufunge kilinda sehemu ya kuingiza karatasi.

  5. Toa trei ya kushikilia nakala zinazochapishwa.

    Kumbuka:

    Rudisha karatasi zinazosalia kwenye paketi. Ukiziwacha katika printa, karatasi hizo zinaweza kukunjika au ubora wa uchapishaji unaweza kupungua.