/ Kuchapisha / Kuchapisha kutoka kwa Kompyuta / Kuchapisha Pande 2 (kwa Windows peke yake)

Kuchapisha Pande 2 (kwa Windows peke yake)

Kiendeshi cha printa huchapisha kiotomatiki kikitenganisha kurasa shufwa na kurasa witiri. Wakati printa hii imemaliza kuchapisha kurasa witiri, geuza karatasi ukifuata maelekezo ya kuchapisha kurasa shufwa. Pina unaweza kuchapisha kijitabu ambacho kinaweza kuundwa kwa kukunja uchapishaji.

Kumbuka:
  • Kipengele hiki hakipatikani kwa uchapishaji usio na mipaka.

  • Ikiwa hutatumia karatasi ambayo inafaa kwa uchapishaji wa pande 2, ubora wa uchapishaji huenda ukapungua na karatasi inaweza kukwama.

  • Kulingana na karatasi na data, wino unaweza kuvuja hadi upande huo mwingine wa karatasi.

  • Ikiwa EPSON Status Monitor 3 imelemazwa, nenda kwa kiendeshi cha printa, bofya Mipangilio Iliyorefushwa katika kichupo cha Utunzaji, na kisha uchague Wezesha EPSON Status Monitor 3.

  • Uchapishaji wa pande 2 huenda usipatikane wakati printa imeunganishwa kupitia mtandao au ni printa inayotumiwa na watu kadhaa.

  1. Weka karatasi katika printa.

  2. Fungua faili unayotaka kuchapisha.

  3. Nenda kwa dirisha la kiendeshi cha printa.

  4. Chagua Mwongozo (Kujalidi ukingo mrefu) au Mwongozo (Kujalidia ukingo mfupi) katika Uchapishaji wa Pande 2 kwenye kichupo cha Kuu.

  5. Bofya Mipangilio, weka mipangilio inayofaa, na kisha ubofye SAWA.

    Kumbuka:

    Iki uchapishe kama kijitabu, chagua Kijitabu.

  6. Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.

  7. Bofya Chapisha.

    Wakati upande wa kwanza umemaliza kuchapishwa, dirisha la kidukizo linaonekana kwenye kompyuta. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini.