/ Kubadilisha Vibweta vya Wino / Kubadilisha Vibweta vya Wino (Wakati Mwangaza wa Wino Umewashwa)

Kubadilisha Vibweta vya Wino (Wakati Mwangaza wa Wino Umewashwa)

Tahadhari:

Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazaji. La sivyo unaweza kujeruhiwa.

Kumbuka:

Iwapo utabadilisha vibweta vya wino unaponakili, nakala asili zinaweza kutoka katika eneo lake. Bonyeza kitufe cha ili kukatisha na kubadilisha nakala asili.

  1. Fungua kitengo cha kitambazaji wakati jalada la waraka limefungwa.

  2. Endesha vitufe vya kichapishi ili kusogeza kishikilio cha kibweta cha wino.

    Kumbuka:

    Badilisha kibweta kinachositisha katika ikoni ya . Iwapo kuna vibweta vya wino vilivyokamilika, kibweta husogezwa kwenye ikoni ya kila wakati unabonyeza kitufe cha .

    • Iwapo mwangaza wa umewashwa (kibweta kimoja au zaidi vya wino vinakamilika)
      Bonyeza kitufe cha . Kishikilio cha kibweta cha wino husonga katika ikoni ya . Huwezi kubadilisha vibweta katika nafasi hii. Nenda kwa hatua inayofuata.
    • Iwapo mwangaza wa umewashwa (kibweta kimoja au zaidi vya wino vinapungua)
      Shikilia kitufe cha chini kwa sekunde 10. Kishikilio cha kibweta cha wino husonga katika ikoni ya . Huwezi kubadilisha vibweta katika nafasi hii. Nenda kwa hatua inayofuata.
    Kumbuka:

    Ili kukatisha ubadilishaji wa wino, endelea kusakinisha vibweta vya wino na uzime kichapishi.

  3. Bonyeza kitufe cha tena.

    Kishikilio cha kibweta cha wino husonga katika nafasi ya ubadilishaji.

  4. Unapobadilisha kibweta cha wino mweusi, tikisa taratibu kibweta kipya cha wino mweusi mara nne au tano na kisha uuondoe kwenye kifurushi chake. Unapobadilisha vibweta vya rangi nyingine, ondoa vibweta vipya vya rangi kutoka kwenye kifurushi chake bila kutikisa.

    Muhimu:

    Usitikise katriji baada ya kufungua pakiti, kwani zinaweza kuvuja.

  5. Ondoa tu utepe wa njano.

    Muhimu:

    Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye picha. Kufanya hivyo kunaweza kuzuia utendaji na uchapishaji wa kawaida.

  6. Minya kichupo kilicho kwenye kibweta cha wino na ukivute moja kwa moja upande wa juu. Iwapo huwezi kuondoa kibweta cha wino, kivute kwa uthabiti.

  7. Chomeka kibweta kipya cha wino, na kisha ukibonyeze chini kwa uthabiti.

  8. Funga kitengo cha kitambazaji.

  9. Bonyeza kitufe cha .

    Kuchaji kwa wino kunaanza.

    Muhimu:

    Baada ya kusakinisha kariji ya wino, taa ya nishati na wino inaendelea kumweka wakati kichapishi kinachaji wino. Usizime printa wakati wa kunyonya wino. Kuchaji kunachukua takriban dakika mbili. Ikiwa unyonyaji wa wino haujakamilika, huwezi kuchapisha.

    Kumbuka:

    Iwapo mwangaza wa hauzimi, jaribu kuondoa na kuchomeka tena kibweta cha wino.