/ Kutatua Matatizo / Wakati Huwezi Kutengeneza Mipangilio ya Mtandao / Wakati Huwezi Kuunganisha Ukitumia Muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi)

Wakati Huwezi Kuunganisha Ukitumia Muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi)

Iwapo tayari idadi ya juu ya vifaa vimeunganishwa, huwezi kuunganisha vifaa vyovyote zaidi. Angalia yafuatayo na ujaribu kuunganisha upya.

Angalia ni vifaa vingapi vimeunganishwa

Angalia ni vifaa vingapi vimeunganishwa kwenye kichapishi. Iwapo idadi ya vifaa vilivyounganishwa haijazidisha kiwango cha juu, huenda kosa la muunganisho limetokea. Sogeza kichapishi na kompyuta au kifaa maizi karibu na kipanga njia pasiwaya ili kusaidia kwa mawasiliano ya mawimbi ya redio, hakikisha kuwa SSID na nenosiri ni sahihi, na kisha jaribu kutengeneza mipangilio ya mtandao tena.

  • Laha la hali ya mtandao

  • Skrini ya hali ya bidhaa kwa Web Config

    Zindua kivinjari cha wavuti kutoka kwenye kifaa kilichounganishwa, na kisha uingize anwani ya IP kwa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) ili kufunguaWeb Config. Donoa Product Status > Wi-Fi Direct na uangalie hali ya Wi-Fi Direct.

Kata muunganisho wa vifaa visivyohitajika

Iwapo tayari idadi ya juu ya vifaa vimeunganishwa kwenye kichapishi, kata muunganisho wa vifaa visivyohitajika na ujaribu kuunganisha kifaa kipya.

Futa SSID kwa Wi-Fi Direct kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa usichohitaji kuunganisha kwenye kichapishi.