/ Kutatua Matatizo / Kuondoa Karatasi Iliyokwama / Kuondoa Karatasi Iliyokwama kutoka Ndani ya Kichapishi

Kuondoa Karatasi Iliyokwama kutoka Ndani ya Kichapishi

Tahadhari:
  • Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazo.La sivyo unaweza kujeruhiwa.

  • Usiwahi kugusa vitufe vilivyo kwenye paneli dhibiti wakati mkono wako uko ndani ya kichapishi.Iwapo kichapishi kitaanza kufanya kazi, kinaweza kusababisha majeraha.Kuwa makini usiguse sehemu zinazojitokeza ili uzuie majeraha.

  1. Fungua kitengo cha kitambazo wakati jalada la waraka limefungwa.

  2. Ondoa karatasi iliyokwama.

    Muhimu:

    Usiguse kebo tambarare nyeupe au sehemu angavu iliyo ndani ya kichapishi.Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

  3. Funga kitengo cha kitambazo.