Kurekebisha Rangi ya Uchapishaji

Unaweza kurekebisha rangi zinazotumiwa katika uchapishaji. Marekebisho haya hayatumiwi kwenye data ya kwanza.

Ubora Picha hutoa picha nzuri zaidi na rangi dhahiri zaidi kwa kurekebisha ulinganuaji, ukifishwaji, na uangavu wa data ya kwanza ya picha kiotomatiki.

Kumbuka:

Ubora Picha hurekebisha rangi kwa kuchanganua eneo la kipengele. Kwa hivyo, ikiwa umebadilisha eneo la kipengele kwa kupunguza, kukuza, kupogoa, au kuzungusha picha hiyo, rangi inaweza kubadilika bila kutarajiwa. Uchaguaji wa mpangilio wa bila-kingo pia hubadilisha eneo la kipengele na husababisha mabadiliko ya rangi. Ikiwa picha iko nje ya mwimo, toni inaweza kuwa sio ya kiasili. Ikiwa rangi imebadilishwa au imekuwa sio ya asili, chapisha kwa modi nyingine mbali na Ubora Picha.

Windows

Chagua mbinu ya kurekebisha rangi katika Usahihishaji wa Rangi kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi.

Ukichagua Otomatiki, rangi zitarekebishwa kiotomatiki ili zilingane na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa uchapishaji. Ukichagua Kaida na ubofye Iliyoboreshwa, unaweza kuweka mipangilio yako mwenyewe.

Mac OS

Nenda kwa mawasiliano ya uchapishaji. Chagua Kulinganisha Rangi katika menyu ya kidukizo, na kisha uchague EPSON Color Controls. Chagua Color Options katika menyu ya kidukizo, na misha uchague moja ya chaguo zinazopatikana. Bofya mshale kando ya Mipangilio Iliyoboreshwa na uweke mipangilio inayofaa.