Msimbo unaonyeshwa kwenye skrini ya LCD iwapo kuna kosa au maelezo yanayohitaji umakinifu wako. Iwapo msimbo umeonyeshwa, fuata suluhisho zifuatazo hapa chini ili kutatua tatizo.
|
Msimbo |
Hali |
Suluhisho |
|---|---|---|
|
E-01 |
Hitilafu ya printa imetokea. |
Fungua kitengo cha kitambazo na uondoe karatasi yoyote au nyenzo yoyote ya kuilinda ndani ya kichapishi. Zima na uwashe printa tena. |
|
E-02 |
Sa la kitambazaji limetokea. |
Zima na uwashe printa tena. |
|
E-12 |
Padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka inahitaji kubadilishwa. |
Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson ili abadilishe padi ya wino ya uchapishaji usio na mipaka*. Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji. Uchapishaji usiokuwa na mpaka haupatikani, lakini kuchapisha mpaka kunapatikana. |
|
W-01 |
Karatasi imekwama. |
Ondoa karatasi kutoka kwenye kichapishi na ubonyeze kitufe kilichoonyeshwa upande wa chini wa skrini ya LCD ili kufuta kosa. Katika hali nyingine, unahitaji kuzima na kuwasha nishati tena. |
|
W-12 |
Vibweta vya wino vimesakinishwa visivyo. |
Bonyeza chini kibweta cha wino kwa nguvu. |
|
W-13 |
Kibweta cha wino kilichoonekana katika skrini ya LCD hakijatambuliwa. |
Badilisha kibweta cha wino. Epson inapendekeza utumie katriji halali za wino za Epson. |
|
W-14 |
Padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake. |
Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson ili abadilishe padi ya wino ya uchapishaji usio na mipaka*. Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji. Ujumbe huu utaendelea kuonekana hadi padi ya wino ibadilishwe. Bonyeza kitufe cha |
|
I-22 |
Weka Wi-Fi kutoka Kitufe cha Msukumo (WPS). |
Sukuma kitufe cha eneo la ufikiaji. Iwapo hakuna kitufe katika eneo la ufikiaji, fungua dirisha la mpangilio wa eneo la ufikiaji, na kisha ubofye kitufe kilichoonekana kwenye programu. |
|
I-23 |
Weka Wi-Fi kutoka Msimbo wa PIN (WPS). |
Ingiza msimbo wa PIN ulioonekana kwenye skrini ya LCD kwenye eneo la ufikiaji au kompyuta ndani ya dakika mbili. |
|
I-31 |
Weka Wi-Fi kutoka M'sho Oto Wi-Fi. |
Sakinisha programu kwenye kompyuta yako, na kisha ubonyeze kitufe cha OK wakati usanidi wa Wi-Fi unaanza. |
|
I-41 |
Ony. Ot. Usan'i/ Kar. imelemazwa. Baadhi ya vitendaji haviwezi kutumika. |
Ikiwa Ony. Ot. Usan'i/ Kar. imelemazwa, huwezi kutumia AirPrint. |
|
I-60 |
Huenda kompyuta yako isiauni WSD (Huduma za Wavuti kwa Vifaa). |
Kipengele cha kutambaza kwenye kompyuta (WSD) kinapatikana tu kwa kompyuta zinazoendesha matoleo ya Kiingereza ya Windows 10, Windows 8.1, Windows 8, Windows 7 au Windows Vista. Hakikisha kuwa kichapishi kimeunganishwa vizuri kwenye kompyuta. |
|
Recovery Mode |
Kichapishi kimeanza katika modi ya kurejesha kwa sababu sasisho la programu msingi halijafaulu. |
Fuata hatua zilizo hapa chini ujaribu kusasisha ngome tena. 1. Unganisha kompyuta na kichapishi ukitumia kebo ya USB. (Wakati wa modi ya kurejesha, huwezi kusasisha programu msingi kupitia muunganisho wa mtandao.) 2. Tembelea tovuti yako ya Epson kwa maelekezo zaidi. |
* Katika baadhi ya mizunguko ya uchapishaji kiasi kidogo sana cha wino wa ziada kinaweza kukusanywa katika padi ya wino. Ili kuzuia uvujaji wa wino kutoka kwa padi, printa hii imeundwa kusimamisha uchapishaji wakati padi imefikisha kikomo chake. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha ukitumia chaguo la kuchapisha bila kingo. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa padi hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Printa itakuarifu wakati padi inahitajika kubadilishwa na jambo linaweza tu kufanywa na Mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu.