/ Chaguo za Menyu kwa Mipangilio / Chaguo za Menyu kwa Usanidi wa Printa

Chaguo za Menyu kwa Usanidi wa Printa

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Mipangilio > Usanidi wa Printa

Mipangilio ya Chanzo cha Karatasi:
Usanidi wa Karatasi:

Chagua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi uliyoingiza katika chanzo cha karatasi.

Ony. Ot. Usan'i/ Kar.:

Teua Washa ili kuonyesha skrini ya Usanidi wa Karatasi unapopakia chanzo cha karatasi. Ukilemaza kipengele hiki, huwezi kuchapisha kutoka kwenye iPhone, iPad au iPod touch ukitumia AirPrint.

Hali Tulivu:

Huenda bidhaa yako isiwe na kipengele hiki kulingana na mahali ulipoinunua.

Teua Washa ili kupunguza kelele wakati wa kuchapisha, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.Kulingana na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa kuchapisha uliyoteua, huenda kusiwe na tofauti katika kiwango cha kelele ya kichapishi.

Kipima Saa ya Kuzima:

Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.

Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.

Mip'ilio ya Kuzima:

Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.

  • Zima Ikiwa Haitumiki

    Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.

  • Zima ikiwa Imetenganishwa

    Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha USB kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.

    Angalia tovuti ifuatayo kwa muda maalum.

    https://www.epson.eu/energy-consumption

Lugha/Language:

Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.

Kibodi

Badillisha muundo wa kibodi kwenye skrini ya LCD.

Kipima saa cha Kulala:

Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.

Muda wa Kukausha Wino:

Teua muda wa kukausha wino unaotaka kutumia unapotekeleza uchapishaji wa pande 2.Kichapishi huchapisha upande mwingine baada ya kuchapisha upande mmoja.Iwapo chapisho lako limepakwa wino, ongeza mpangilio wa muda.