/ Kunakili / Chaguo za Menyu kwa Kunakili

Chaguo za Menyu kwa Kunakili

Kumbuka:

Menyu zinazopatikana hutofautiana kulingana na mpangilio unaochagua.

Idadi ya nakala:

Ingiza idadi ya nakala.

Rangi:

Hunakili nakala asili katika rangi.

Ny'i&N'pe:

Hunakili nakala asili katika rangi nyeusi na nyeupe (rangi moja).

Pande 2:
  • 1>Upande 1

    Hunakili upande mmoja wa hati halisi kwenye karatasi ya upande moja.

  • 1>Pande 2

    Hunakili hati halisi zenye pande mbele kwenye pande mbili za karatasi moja.

Uzito:

Ongeza kiwango cha uzito kwa kubonyeza kitufe cha wakati matokeo ya kunakili ni hafifu. Punguza kiwango cha uzito kwa kubonyeza kitufe cha wakati wino unaharibika.

Punguza/Ongeza:

Hukuza au kupunguza nakala asili.

  • Ukubwa Halisi

    Hunakili kwa ukuzaji wa 100%.

  • Tosheza Kiotomati

    Hutambua eneo la kuchapisha na kukuza kiotomatiki au kupunguza nakala asili ili itoshee kwenye ukubwa wa karatasi uliyoteua. Wakati kuna pambizo nyeupe kwenye nakala asili, pambizo hizo nyeupe kutoka kwenye alama ya kona ya kioo cha kitambazaji zinatambuliwa kama eneo la kutambaza, lakini pambizo katika upande mkabala zinaweza kupunwa.

  • Maalum

    Teua ili kubainisha ukuzaji ili kuongeza au kupunguza nakala asili.

Ukubwa Maalum:

Hubainisha ukuzaji unaotumika kuongeza au kupunguza nakala asili ndani ya masafa ya 25 hadi 400%.

Mipangilio ya K'si:

Weka ukubwa na aina ya karatasi uliyoweka Kuchapisha katika kichapishi.

Kurasa Nyingi:
  • Ukurasa Mmoja

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.

  • 2-juu

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.

Ubora:

Teua ubora wa kuchapisha. Kuteua Bora hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini.

Kwa watumiaji wa Ulaya Magharibi, modi ya mswadajaribio haipatikani.

Upanuzi:

Kwa uchapishaji usio na mpaka, taswira inakuzwa kiasi ili kuondoa mipaka kutoka kwa kingo za karatasi. Teua kiwango cha kukuza taswira.