/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Kiendeshi cha Kichapishi cha Windows

Kiendeshi cha Kichapishi cha Windows

Kiendeshi cha kichapishi hudhibiti printa kulingana na amri za programu. Kuweka mipangilio kwenye kiendeshi cha kichapishi hutoa matokeo bora zaidi ya uchapishaji. Pia unaweza kuangalia hali ya kichapishi au kuiweka ikiwa katika hali nzuri kwa kutumia huduma ya kiendeshi cha kichapishi.

Kumbuka:

Unaweza kubadilisha lugha ya kiendeshi cha kichapishi. Teua lugha unayotaka kutumia kutoka kwa mpangilio wa Lugha kwenye kichupo cha Utunzaji.

Kufikia kiendeshi cha kichapishi kutoka kwa programu-tumizi

Ili uweke mipangilio inayotumika kwenye programu unayotumia peke yake, ifikie kutoka kwa programu hiyo.

Chagua Chapisha au Usanidi wa Uchapishaji katika menyu ya Faili. Chagua printa yako, na kisha ubofye Mapendeleo au Sifa.

Kumbuka:

Utendaji hutofautiana kulingana na programu. Angalia msaada wa programu kwa maelezo.

Kufikia kiendeshi cha printa kutoka kwa paneli dhibiti

Kuweka mipangilio inayotumika kwenye programu zote, ifikie kutoka kwa paneli dhibiti.

  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Mfumo wa Windows > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na kichapishi kwenye Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uteue Mapendeleo ya uchapishaji.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Teua Eneo Kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na kichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uchague Mapendeleo ya uchapishaji.

  • Windows 7

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na kichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.

  • Windows Vista

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Kichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Teua mapendeleo ya uchapishaji.

  • Windows XP

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Vichapishi na Maunzi Nyingine > Vichapishi na Faksi. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.

Kufikia kiendeshi cha printa kutoka kwa ikoni ya printa kwenye mwambaa kazi

Ikoni ya printa iliyo kwenye mwambaa kazi wa eneo kazi ni ikoni ya mkato ya kukuwezesha ufikie kiendeshi cha printa kwa urahisi.

Ukibofya ikoni ya printa na uchague Mipangilio ya Printa, unaweza kufikia dirisha sawa la mipangilio ya printa na linaloonekana katika paneli dhibiti. Ukibofya ikoni hii mara mbili, unaweza kuona hali ya printa.

Kumbuka:

Ikiwa ikoni ya printa haionekani kwenye mwabaa kazi, nenda kwa dirisha la kiendeshi cha printa, bofya Inachunguza Mapendeleo kwenye kichupo cha Utunzaji, na kisha uchague Sajili ikoni ya njiamkato kwenye upau kazi.

Kuanzisha huduma

Nenda kwa dirisha la kiendeshi cha kichapishi. Bofya kichupo cha Utunzaji.