/ Utambazaji / Utambazaji Kupitia Paneli Dhibiti / Utambazaji kwa Kompyuta

Utambazaji kwa Kompyuta

Unaweza kuhifadhi taswira iliyotambazwa kwenye kompyuta.

Muhimu:

Hakikisha umesakinisha Epson Scan 2 na Epson Event Manager kwneye kompyuta yako kabla ya kutumia kipengele hiki.

  1. Weka nakala za kwanza.

  2. Ingiza Changanua kutoka kwenye skrini ya mwanzo kwa kutumia kitufe cha au , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  3. Teua jinsi ya kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kompyuta kutoka kwenye menyu zifuatazo kwa kutumia kitufe cha au , na kisha kubonyeza kitufe cha OK.

    • Kwenye Kompyuta (JPEG): Huhifadhi picha iliyotambazwa kwenye umbizo la JPEG.
    • Kwenye Kompyuta (PDF): Huhifadhi picha iliyotambazwa kwenye umbizo la PDF.
    • Kwenye Kompyuta (Barua pepe): Huanzisha huduma ya barua pepe ya mteja kompyuta, na kisha huiambatisha kiotomatiki kwenye barua pepe.
    • Kwenye Kompyuta (Maalum): Huhifadhi picha iliyotambazwa kwa kutumia mipangilio kwenye Epson Event Manager. Unaweza kubadilisha mipangilio ya utambazaji kama vile ukubwa wa kutambaza, kabrasha la kuhifadhi, au umbizo la kuhifadhi.
  4. Teua kompyuta unayotaka kuhifadhi picha zilizotambazwa.

    Kumbuka:
    • Unaweza kubadilisha mipangilio ya utambazaji kama vile ukubwa wa kutambaza, kabrasha la kuhifadhi, au umbizo la kuhifadhi, kwa kutumia Epson Event Manager.

    • Wakati kichapishi kimeunganishwa kwenye mtandao, unaweza kuteua kompyuta ipi ambayo unataka kuhifadhi taswira iliyotambazwa. Hadi kompyuta 20 zinaweza kuonekana kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    • Wakati kompyuta unayotaka kuhifadhi picha zilizotambazwa imegunduliwa kwenye mtandao, vibambo 15 vya kwanza vya jina la komyuta vinaonekana kwenye paneli dhibiti. Iwapo utaweka Network Scan Name (Alphanumeric) kwenye Epson Event Manager, inaonyeshwa katika paneli dhibiti.

  5. Bonyeza kitufe cha .

    Kumbuka:

    Rangi, ukubwa, na ukingo wa taswira iliyotambazwa hautakuwa sawa na asili.