/ Kuchapisha / Kuchapisha kutoka kwa Kompyuta / Kuchapisha Pande 2 / Uchapishaji wa Pande 2 — Mac OS

Uchapishaji wa Pande 2 — Mac OS

  1. Weka karatasi katika kichapishi.

  2. Fungua faili unayotaka kuchapisha.

  3. Fikia kidadisi cha uchapishaji.

  4. Teua Two-sided Printing Settings kutoka kwa menyu ibukizi.

  5. Teua zinazofungana kwenye Two-sided Printing.

  6. Teua aina ya asili kwenye Document Type.

    Kumbuka:
    • Huenda uchapishaji ukapungua kasi kulingana na mpangilio wa Document Type.

    • Iwapo unachapisha data yenye uzito wa juu kama vile picha au grafu, teua M. yaliyo na Picha au Photo kamampangilio wa Document Type.Ikiwa kuchakaa kutatokea au picha ivuje wino upande wa nyuma, rekebisha uzito wa chapa na muda wa wino kukauka kwa kubofya alama ya kishale kando ya Adjustments.

  7. Weka vipengele hivyo vingine inavyohitajika.

  8. Bofya Chapisha.