Mipangilio ya Faksi

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Faksi > Mipangilio ya Faksi

Mipangilio ya Utambazaji:
  • Ukubwa Asili (Glasi)

    Teua ukubwa na uelekeo wa waraka halisi uliyowekwa kwenye glasi ya kichanganuzi.

  • Hali ya Rangi

    Teua iwapo utatambaza kwenye rangi au katika monokromu.

  • Mwonekano

    Teua mwonekano wa faksi inayotoka.

  • Uzito

    Huweka uzito wa faksi inayotoka.

  • Ondoa Mand'yuma

    Hutambua rangi ya karatasi (rangi ya mandharinyuma) ya waraka asili, na kuondoa au kuweka rangi kuwa hafifu. Kulingana na ukolevu na uwazi wa rangi, inaweza kuondolewa au kufanywa kuwa hafifu

  • Uta'ji Unao'a ADF

    Wakati unatuma faksi kutoka kwenye ADF, huwezi kuongeza hati halisi katika ADF, baada ya kuanzisha uchanganuzi. Ukiweka hati halisi zenye ukubwa tofauti katika ADF, hati zote halisi hutumwa kwa ukubwa wa juu zaidi kati ya hizo. Wezesha chaguo hili ili printa ikuulize ikiwa unataka kuchanganua ukurasa mwingine baada ya hati halisi katika ADF imemaliza kuchanganua. Kisha unaweza kuchambua na kuchanganua hati zako halisi kwa ukubwa na kuzituma kama faksi moja.

Mipangilio ya Kutuma Faksi:
  • Tuma Moja kwa Moja

    Hutuma faksi za rangi moja kwa mpokeaji mmoja punde tu muunganisho unapofanywa, bila kuhifadhi picha iliyochanganuliwa kwenye kumbukumbu. Ukikosa kuwezesha chaguo hili, printa huanza kupitisha baada ya kuhifadhi picha iliyochanganuliwa kwenye kumbukumbu na inaweza kusababisha hitilafu ya kumbukumbu kujaa wakati wa kutuma kurasa nyingi. Kwa kutumia chaguo hili, unaweza kuepuka hitilafu, lakini huchukua muda mrefu zaidi kutuma faksi. Huwezi kutumia chaguo hili wakati unatuma faksi kwa wapokeaji wengi.

  • Tuma Faksi Baadaye

    Hutuma faksi wakati ambao ulibainisha. Faksi ya rangi moja tu ndio inayopatikana wakati unatumia chaguo hili.

  • Ongeza Maelezo ya Mtumaji

    • Ongeza Maelezo ya Mtumaji:

      Teua eneo ambalo unataka kujumuisha maelezo ya kijajuu (jina la mtumaji na nambari ya faksi) kwenye faksi inayoondoka, au kutojumuisha maelezo.

      - Zima: Hutuma faksi isiyokuwa na maelezo ya kijajuu.

      - Nje ya Picha: Hutuma faksi pamoja na maelezo ya kijajuu katika pambizo nyeupe ya juu ya faksi. Hii huzuia kijajuu kupitana na taswira iliyotambazwa, hata hivyo, faksi iliyopokewa na mpokeaji inaweza kuchapishwa katika laha mbili kulingana na ukubwa wa nakala asili.

      - Ndani ya Picha: Hutuma faksi kwa maelezo ya kijajuu karibu 7 mm chini kuliko upande wa juu wa taswira iliyotambazwa. Kijajuu kinaweza kupitana na taswira, hata hivyo, faksi iliyopokewa na mpokeaji haitagawanywa kwa nyaraka mbili.

    • Kijajuu cha Faksi:

      Teua kijajuu kwa mpokeaji. Ili kutumia kipengele hiki, lazima usajili vijajuu anuwai mapema.

    • Maelezo ya Ziada:

      Teua maelezo unayotaka kuongeza. Unaweza kuteua moja kutoka kwa Nambari Yako ya Simu na Orodha ya Mfikio.

  • Ripoti ya Upitishaji

    Huchapisha ripoti ya utumaji kiotomatiki baada ya wewe kutuma faksi. Chagua Chapisha Hitilafu Ikitokea ili uchapishe ripoti peke yake wakati hitilafu inatokea. Iwapo Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Ripoti > Ambatisha Tasw. Faksi kwenye ripoti imewekwa, taswira ya waraka inachapishwa kwa ripoti.

  • Ondoa Mipangilio Yote

    Hurejesha mipangilio yote kwenye Mipangilio ya Faksi hadi chaguo-msingi yake.