/ Kutuma Faksi / Kuweka Faksi / Kuweka Mipangilio Msingi ya Faksi / Kuweka Mipangilio Msingi ya Faksi Ukitumia Sogora ya Mpangilio wa faksi

Kuweka Mipangilio Msingi ya Faksi Ukitumia Sogora ya Mpangilio wa faksi

Weka mipangilio msingi kwa kufuata maelekezo yaliyo kwenye skrini.

  1. Unganisha klivhapishi kwenye laini ya simu.

    Kumbuka:

    Kwa sababu ukaguzi wa muunganisho otomatiki wa faksi hufanywa mwisho wa sogora, hakikisha umeunganisha printa kwenye laini ya simu kabla ya kuanzisha sogora.

  2. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.

  3. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Sogora ya Mpangilio wa faksi.

  4. Kwenye skrini ya Sogora ya Mpangilio wa faksi, donoa Endelea.

    Sogora inaanza.

  5. Kwenye skrini ya kuingiza kichwa cha faksi, ingiza jina lako la mtumaji kama vile jina la kampuni yako, na kisha udonoe OK.

    Kumbuka:

    Jina lako la mtumaji na nambari yako ya faksi inaonekana kama kichwa kwenye faksi inayotoka.

  6. Kwenye skrini ya kuingiza nambari ya simu, ingiza nambari yako ya faksi, na kisha udonoe OK.

  7. Kwenye skrini ya Mipangilio ya Distinctive Ring Detection (DRD), weka mipangilio ifuatayo.

    • Ikiwa umejisajili kwa huduma ya mzunguko tofauti kutoka kwa kampuni yako ya simu: Teua Mipangilio, na kisha uteue ruwaza ya mlio ya kutumiwa kwa faksi zinazoingia.
      - Iwapo utateua Zote, nenda kwenye hatua ya 8.
      - Iwapo utateue mpangilio wowote mwingine, Hali ya Kupokea imewekwa otomatiki kwa Otomatiki.Nenda kwenye hatua ya 10.
    • Iwapo huhitaji kuweka chaguo hili: Donoa Ruka, na kisha uende kwenye hatua ya 10.
    Kumbuka:
    • Huduma tofauti za mzunguko, zinazotolewa na makampuni mengi ya simu (jina la huduma hutofautiana na kampuni), hukuwezesha kuwa na nambari kadhaa za simu kwenye laini moja ya simu.Kila nambari inapewa ruwaza tifauti ya mzunguko.Unaweza kutumia nambari moja kwa simu za sauti na nyingine kwa simu za faksi.Chagua ruwaza ya mzunguo iliyopewa kwa simu za faksi katika DRD.

    • Kulingana na eneo, Washa na Zima huonekana kama chaguo za DRD.Chagua Washa ili utumie kipengele tofatui cha mzunguko.

  8. Kwenye skrini ya Mpangilio wa Hali ya Kupokea, chagua kama unatumia kifaa chako cha simu kilichounganishwa kwenye printa.

    • Wakati umeunganishwa: Teua Ndiyo, na uende kwenye hatua inayofuata.
    • Wakati haijaunganishwa: Teua La na uende kwenye hatua ya 10.Hali ya Kupokea imewekwa kwenye Otomatiki.
  9. Kwenye skrini ya Mpangilio wa Hali ya Kupokea, chagua kama unataka kupokea faksi kiotomatiki.

    • Ili upokee kiotomatiki: Teua Ndiyo.Hali ya Kupokea imewekwa kwenye Otomatiki.
    • Ili upokee kikuli: Teua La.Hali ya Kupokea imewekwa kwenye Mwenyewe.
  10. Kwenye skrini ya Endelea, kagua mipangilio uliyofanya, na kisha udonoe Endelea.

    Ili kurekebisha au kubadilisha mipangilio, donoa .

  11. Teua Anza Kukagua ili uendeshe ukaguzi wa muunganisho wa faksi, na skrini inapokuuliza uchapishe matokeo ya ukaguzi, teua Chapisha.

    Ripoti ya matokeo ya ukaguzi inayoonyesha hali ya muunganisha imechapishwa.

    Kumbuka:
    • Ikiwa kuna hitilafu zozote ambazo zimeripotiwa, fuata maelekezo yaliyo kwenye ripoti ili uzitatue.

    • Ikiwa skrini ya Chagua Aina ya Laini imeonyeshwa, chagua aina ya laini.

      - Wakati unaunganisha kichapishi kwenye mfumo wa simu wa PBX au adapta ya taminali, teua PBX.

      - Unapounganisha kichapishi kwenyue laini wastani ya simu, teua PSTN, na kisha uteue Usigundue kwenye skrini iliyoonyeshwa ya Thibitisho.Hata hivyo, kuweka hii kwa Usigundue kunaweza kusababisha printa iruke tarakimu ya kwanza ya nambari ya faksi wakati wa kudayo na itume faksi kwa nambari isiyo sahihi.