Kutuma faksi kwa Kijajuu Kilichoteuliwa

Unapotuma faksi, unaweza kuteua maelezo ya kijajuu kutoka kwa mpokeaji.Ili kutuymia kipengele hiki, lazima usajili vijajuu anuwai mapema.

  1. Teua Faksi kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Chagua Mipangilio ya Faksi > Ongeza Maelezo ya Mtumaji.

  3. Teua mahali unataka kuongeza maelezo yako ya mtumaji.

    • Zima: Hutuma faksi isiyokuwa na maelezo ya kijajuu.
    • Nje ya Picha: Hutuma faksi pamoja na maelezo ya kijajuu katika pambizo nyeupe ya juu ya faksi.Hii huzuia kijajuu kupitana na taswira iliyotambazwa, hata hivyo, faksi iliyopokewa na mpokeaji inaweza kuchapishwa katika laha mbili kulingana na ukubwa wa nakala asili.
    • Ndani ya Picha: Hutuma faksi kwa maelezo ya kijajuu karibu mm 7 chini kuliko upande wa juu wa taswira iliyotambazwa.Kijajuu kinaweza kupitana na taswira, hata hivyo, faksi iliyopokewa na mpokeaji haitagawanywa kwa nyaraka mbili.
  4. Teua uga wa Kijajuu cha Faksi, na kisha uteue kijajuu unachotaka kutumia.

  5. Donoa mojawapo ya chaguo Maelezo ya Ziada kama inavyohitajika.

  6. Teua OK ili kutekeleza mipangilio.