/ Kuchapisha / Kuchapisha Kutoka kwa Vifaa Mahiri / Kuchapisha kwa Kugusa Vifaa Maizi kwenye Lebo ya NFC

Kuchapisha kwa Kugusa Vifaa Maizi kwenye Lebo ya NFC

Unaweza kuunganisha kichapishi na kifaa chako maizi kiotomatiki na uchapishe kwa kugusa antena ya NFC ya kifaa maizi kinachoendesha Android 4.0 au baadaye na hiyo huauni NFC (Near Field Communication) kwenye lebo ya NFC ya kichapishi.

Eneo la antena la NFC hutofautiana kulingana na kifaa maizi. Tazama waraka uliotolewa kwa kifaa chako maizi kwa maelezo zaidi.

Muhimu:
  • Hakikisha kuwa mpangilio wa muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) umewezeshwa.

  • Wezesha kitendaji cha NFC kwenye kifaa chako maizi.

  • Hakikisha kuwa Epson iPrint imesakinishwa kwenye kifaa chako maizi. Iwapo sivyo, gusa antena ya NFC ya kifaa maizi kwenye lebo ya NFC ya kichapishi na ukisakinishe.

Kumbuka:
  • Iwapo kichapishi hakiwasiliana na kifaa maizi hata baada ya kukigusa kwenye lebo, jaribu kurekebisha mkao wa kifaa maizi na ukiguse kwenye lebo tena.

  • Iwapo kuna vuzuizi kama vile chuma katikati ya lebo ya NFC ya kichapishi na antena ya NFC ya kifaa maizi, huenda kichapishi kisiweze kuwasiliana na kifaa maizi.

  • Kipengele hiki hutumia muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) ili kuunganisha kwenye kichapishi. Unaweza kuunganisha hadi vifaa vinne kwenye kichapishi kwa wakati mmoja.

  • Iwapo umebadilisha nenosiri la muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi), huwezi kutumia kipengele hiki. Weka upya nenosiri la kwanza ili kutumia kipengele hiki.

  1. Weka karatasi katika kichapishi.

  2. Gusa antena ya NFC ya kifaa chako maizi kwenye lebo ya NFC ya kichapishi.

    Epson iPrint huanza.

  3. Kwenye skrini ya nyumbani ya Epson iPrint, gusa antena ya NFC ya kifaa chako maizi kwenye lebo ya NFC ya kichapishi tena.

    Kichapishi na kifaa maizi vimeunganishwa.

  4. Teua taswira unayotaka kuchapidsha, na kisha uteue Next upande wa juu kulia wa skrini.

  5. Gusa antena ya NFC ya kifaa chako maizi kwenye lebo ya NFC ya kichapishi tena.

    Uchapishaji unaanza.