Zaidi

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Faksi > (Zaidi)

Kumbukumbu ya Upitishaji:

Unaweza kukagua historia ya kazi zilizotumwa au zilizopokewa za faksi.

Ripoti ya Faksi:
  • Upitishaji wa Mwisho

    Huchapisha ripoti ya faksi ya awali iliyotumiwa au kupokewa kupitia uchaguzi.

  • Kumbukumbu ya Faksi

    Huchapisha ripoti ya usambazaji.Unaweza kuweka ichapishe hii ripoti kiotomatiki ukitumia menyu ifuatayo.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Ripoti > Chapisha Otomatiki Batli ya Faksi

  • Mipangilio ya Orodha ya Faksi

    Huchapisha mipangilio ya sasa ya faksi.

  • Ufuatiliaji Itifaki

    Huchapisha ripoti kamili ya faksi ya awali iliyotumwa au kupokewa.

Itisha Hati:

Huunganisha kwenye nambari ya faksi uliyoingiza na hupokea faksi iliyohifadhiwa kwenye mashine ya faksi.Unaweza kutumia chaguo hili kupokea fasi kutoka kwa huduma ya maelezo ya faksi.

Kisanduku pokezi:

Hufungua kikasha pokezi ambacho faksi zilizopokewa huhifadhiwa.

Chapisha tena faksi iliyopokewa:

Huchapisha tena faksi zilizopokewa.

Mipangilio ya Faksi:

Hufungua Mipangilio ya Faksi.Pia unaweza kufikia skrini hii kwa kuteua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani, na kisha kuteua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi.Kwa maelezo zaidi, angalia ukurasa unaofafanua kipengele cha Mipangilio ya Faksi.