/ Kutuma Faksi / Kupokea Faksi kwenye Kichapishi / Kuweka Modi ya Kupokea

Kuweka Modi ya Kupokea

Unaweza kuunda Hali ya Kupokea kwa kutumia Sogora ya Mpangilio wa faksi. Unapounda mpangilio wa faksi kwa mara ya kwanza, tunapendekeza utumie Sogora ya Mpangilio wa faksi. Iwapo unataka kubadilisha tu Hali ya Kupokea, fuata maagizo yaliyo hapa chini.

  1. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Hali ya Kupokea.

  3. Teua Hali ya Kupokea kulingana na matumizi yako.

    Muhimu:

    Iwapo simu haijaunganishwa, lazima uteue Otomatiki.

    • Kutumia laini ya simu pekee kwa faksi:
      Teua Otomatiki.
      Hubadili kiotomatiki ili kupokea faksi wakati idadi ya milio uliyoweka kwenye Hutoa mlio ili Kujibu imekamilika.
      Kumbuka:

      Tunapendekeza kuweka Hutoa mlio ili Kujibu kwa idadi ya chini iwezekanavyo.

    • Kutumia lani moja ya simu kwa simu zinazopigwa na faksi (hususan kwa utumaji faksi):
      Teua Otomatiki.
      Hubadili kitomatiki ili kupokea faksi wakati idadi ya milio uliyoweka kwenye Hutoa mlio ili Kujibu imefika.
      Kumbuka:

      Unaweza kupiga simu ya sauti iwapo utakata simu ndani ya idadi ya milio iliyowekwa kwenye Hutoa mlio ili Kujibu.

    • Kutumia laini moja ya simu kwa simu na faksi (hasa kwa upigaji simu):
      Teua Mwenyewe.
      Unaweza kujibu simu kwa kifaa cha nje cha simu. Unapotuma faksi, unaweza kuanza kupokea faksi kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapsihi.
      Kumbuka:

      Unapounda mipangilio ya Pokea kwa Mbali, unaweza kuanza kupokea faksi kwa kutumia operesheni zilizounganishwa kwenye simu pekee.