Kutuma Faksi kwa Kutumia Paneli Dhibiti

Unaweza kutuma faksi kwa kuingiza nambari za faksi kwa wapokeaji kwa kutumia paneli dhibiti. Kichapishi hupigia wapokeaji kiotomatiki na kutuma faksi.

  1. Weka nakala za kwanza.

    Kumbuka:

    Unaweza kutuma kurasa 100 kwa utumaji mmoja; hata hivyo kulingana na kiwango cha kumbukumbu kinachobakia, huenda usiwezi kutuma faksi iliyo na chini ya kurasa 100.

  2. Teua Faksi kwenye skrini ya nyumbani.

  3. Bainisha mpokeaji.

    Unaweza kutuma fakdsi sawa ya monokromu kwa hadi wapokeaji 100 ukijumuisha hadi vikundi 99 kwenye Waasiliani. Hata hivyo, rangi ya faksi inaweza kutumwa tu kwa mpokeaji mmoja kwa wakati mmoja.

    • Ili kuingiza kikuli: Teua Kibodi, ingiza nambari ya faksi kwenye skrini inayoonyeshwa, na kisha udonoe OK.
      - Ili kuongeza kusitisha (sitisha kwa sekunde tatu wakati wa kupiga) ingiza kistari kifupi(-).
      - Ikiwa utaweka msimbo wa ufikiaji wa nje katika Aina ya Laini, ingizar “#” (hashi) badala ya msimbo wa ufikiaji wa nje mwanzoni wa nambari ya faksi.
    • Ili kuteua kutoka kwenye orodha ya waasiliani: Teua Waasiliani na uongeze alama ya tiki kwenye mwasiliani. Iwapo bado wapokeaji unaotaka kuwatumia hawajasajiliwa kwenye Waasiliani, unaweza kumsajili mpokeaji kwanza kwa kuteua Ongeza Ingizo.
    • Ili kuteua kutoka kwenye historia ya faksi iliyotumwa: Teua Hivi karibuni, na kisha uteue mpokeaji.
    Kumbuka:
    • Wakati Vikwazo vya Kupiga Moja kwa moja kwenye Mipangilio ya Usalama imewekwa kwa On, unaweza kuteua tu wapokeaji wa faksi kutoka kwenye orodha ya waasiliani au historia ya faksi iliyotumwa. Huwezi kuingiza nambari ya faksi kwa mikono.

    Ili kufuta wapokeaji uliowaingiza, onyesha orodha ya wapokeaji kwa kudonoa sehemu kwenye skrini ambayo inaonyesha nambari ya faksi au iidadi ya wapokeaji kwenye skrini ya LCD, teua mpokeaji kutoka kwenye orodha, na kisha uteue Ondoa.

  4. Teua kichupo cha Mipangilio ya Faksi, na kisha uweke mipangilio kama vile mwonekano na mbinu ya utumaji inavyohitajika.

  5. Teua kichupo cha Mpokeaji, na kisha utume faksi.

    • Ili kutuma bila kuangalia picha ya waraka uliotambazwa: Donoa .
    • Ili kutambaza, angalia picha ya waraka uliotambazwa, na kisha utume (wakati utumaji faksi ni wa monokromu pekee): Teua Hakiki kwenye kichupo cha Mpokeaji.
      Ili kutuma faksi jinsi ilivyo, teua Anza Kutuma. Vinginevyo, katisha uhakiki kwa kuteua Ghairi, na kidsha uende kwenye hatua ya 3.

    - : Husogeza skrini katika mwelekeo wa vishale.

    - : Hupunguza au kuongeza.

    - : Husonga kwa ukurasa wa awali au unaofuata.

    Kumbuka:
    • Huwezi kutuma faksi kwa rangi baada ya kuhakiki.

    • Wakati Tuma Moja kwa Moja imewezeshwa, huwezi kuhakiki.

    • Wakati skrini ya kuhakiki isipoguzwa kwa sekunde 20, faksi hutmwa kiotomatiki.

    • Ubora wa picha wa faksi iliyotumwa huenda ukawa tofauti na ulichohakiki kulingana na uwezo wa mashine ya mpokeaji.

  6. Wakati utumaji umekamilika, ondoa nakala asili.

Kumbuka:
  • Ikiwa nambari ya faksi ina shughuli au tatizo litokee, printa hudayo upya mara mbili kiotomatika baada ya dakika moja.

  • Ili kukatisha utumaji, donoa .

  • Huchukua muda murefu kutuma faksi ya rangi kwa sababu printa hufanya utambazaji na utumaji kwa wakati mmoja. Wakati kichapishi kinatuma faksi ya rangi, huwezi kutumia vipengele vingine.