/ Mambo Msingi ya Uchapishaji / Mwongozo wa Paneli Dhibiti / Mwongozo wa Skrini ya Nyumbani

Mwongozo wa Skrini ya Nyumbani

Huonyesha vipengee ambavyo vimesanidiwa kwa kichapishi kama ikoni. Teua ikoni kwa kubonyeza vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK ili kuangalia mipangilio ya sasa au kufikia kila menyu ya mpangilio.

Huonyesha kila menyu.

Nakili

Hukuruhusu kunakili waraka.

Changanua

Hukuruhusu kutambaza waraka au picha.

Faksi

Hukuruhusu kutuma faksi.

Matengenezo

Huonyesha menyu zinazopendekezwa kuimarisha ubora wa machapisho yako kama vile kuzibua nozeli kwa kuchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli na kutekeleza usafishaji wa kichwa, na kuboresha ukungu au mistari kwenye machapisho yako kwa kupangilia kichwa cha kuchapisha. Hii ni njia mkato kwa menyu ifuatayo.

Mipangilio > Matengenezo

Mipangilio

Hukuruhusu kuunda mipangilio inayohusiana na matengenezo, usanidi wa kichapishi, na mipangilio ya mtandao.

Huonyesha skrini ya Maelezo ya Data ya Faksi.

Unaweza kubiringiza kulia kwa kubonyeza kitufe cha .