/ Mipangilio ya Mtandao / Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwenye Kichapishi / Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Kuingiza SSID na Nenosiri

Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Kuingiza SSID na Nenosiri

Unaweza kusanidi kikuli mtanfdao wa Wi-Fi kwa kuingiza maelezo muhimu ya kuunganisha kwenye kipanga njia pasiwaya kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Ili kusanidi kwa kutumia mbinu hii, unahitaji SSID na nenosiri kwa kipanga njia pasiwaya.

Kumbuka:

Iwapo unatumia eneo la kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio yake chaguo-msingi, SSID na nywila ziko kwenye lebo. Iwapo hufahamu SSID na nywila, tazama nyaraka zilizotolewa na kipanga njia pasiwaya.

  1. Teua kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Wi-Fi (Inapendekezwa).

  3. Bonyeza kitufe cha OK ili kuonyesha skrini inayofuata.

    Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Teua Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.

  4. Teua Sogora ya Kusanidi Wi-Fi.

  5. Teua SSID kwa kipanga njia pasiwaya.

    Kumbuka:
    • Iwapo SSID unayotaka kuunganisha kwayo haionyeshwi kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, bonyeza ili kusasisha orodha. Iwapo bado haitaonyeshwa, teua , na kisha uingize SSID moja kwa moja.

    • Iwapo hujui jina la mtandao (SSID) angalia iwapo maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Iwapo unatumia kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio yake chaguo-msingi, tumia SSID kwenye lebo. Iwapo huwezi kutafuta maelezo yoyote, tazama nyaraka zilizotolewa pamoja na kipanga njia pasiwaya.

  6. Bonyeza kitufe cha Sawa, na kisha uingize nenosiri.

    Kumbuka:
    • Nenosiri linaathiriwa na herufi ndogo na kubwa.

    • Iwapo hujui nenosiri, angalia iwapo maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia pasiwaya. Kwenye lebo, nenosiri linaweza kuandikwa “Network Key”, “Wireless Password”, na kadhalika. Iwapo unatumia kipanga njia pasiwaya kwa mipangilio chaguo-msingi, tumia nenosiri lililoandikwa kwenye lebo.

  7. Unapokamilisha, teua OK.

  8. Angalia mipangilio, na kisha uteue Anza Kusanidi.

  9. Teua Puuza ili kukamilisha.

    Kumbuka:

    Ukishindwa kuunganisha, pakia karatasi tupu la ukubwa wa A4, na kisha uteue Chapisha Ripoti ya Ukaguzi ili kuchapisha ripoti ya muunganisho.

  10. Bonyeza kitufe cha .