/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Programu-tumizi ya Kusanidi Operesheni za Kichapishi (Web Config)

Programu-tumizi ya Kusanidi Operesheni za Kichapishi (Web Config)

Web Config ni programu ambayo huendeshwa katika kivinjari cha wavuti, kama vile Internet Explorer na Safari, kwenye kompyuta na kifaa mahiri. Unaweza kuthibitisha hali ya printa au kubadilisha huduma ya ntandao na mipangilio ya printa. Ili utumie Web Config, unganisha printa na kompyuta au kifaa kwenye mtandao mmoja.

Vivinjari vifuatavyo vinakubaliwa.

Programu Endeshi

Kivinjari

Windows XP SP3 au mpya

Microsoft Edge, Internet Explorer 8 au toleo la baadaye, Firefox*, Chrome*

Mac OS X v10.6.8 au mpya

Safari*, Firefox*, Chrome*

iOS*

Safari*

Android 2.3 au mpya

Kivinjari msingi

Chrome OS*

Kivinjari msingi

* Tumia toleo lipya.