Kuendesha Web Config kwenye Windows

Unapounganisha kompyuta kwenye kichapishi kwa kutumia WSD, fuata hatua hapa chini ili kuendesha Web Config.

  1. Fungua orodha ya vichapishi kwenye kompyuta.

    • Windows 10/Windows Server 2016
      Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Mfumo wa Windows > Paneli Dhibiti > Tazam vifaa na vichapishi kwenye Maunzi na Sauti.
    • Windows 8.1/Windows 8/Windows Server 2012 R2/Windows Server 2012
      Teua Eneo-kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na kichapishi katika Maunzi na Sauti (au Maunzi).
    • Windows 7/Windows Server 2008 R2
      Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli ya Udhibiti > Tazama vifaa na kichapishi katika Maunzi na Sauti.
    • Windows Vista/Windows Server 2008
      Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Kichapishi katika Maunzi na Sauti.
  2. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Sifa.

  3. Teua kichupo cha Huduma ya Wavuti na ubofye URL.