Mipangilio Msingi

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi

Sauti:

Rekebisha sauti.

  • Nyamazisha

    Teua On ili kunyamazisha sauti.

  • Hali ya Kawaida

    Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe.

  • Hali Tulivu

    Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe kwenye Hali Tulivu.

Kipima saa cha Kulala:

Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.

Kipima Saa ya Kuzima:

Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.

Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.

Mip'ilio ya Kuzima:

Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.

  • Zima Ikiwa Haitumiki

    Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.

  • Zima ikiwa Imetenganishwa

    Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi baada ya dakika 30 wakati vituo tarishi vyote vinajumuisha kituo tayarishi cha LINE vimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.

Mipangilio ya Tarehe/Saa:
  • Tarehe/Saa

    Ingiza tarehe na saa ya sasa.

  • Saa za Mchana Mrefu

    Teua mpangilio wa wakati wa majira ya joto unaotumika katika eneo lako.

  • Utofauti wa Saa

    Ingiza tofauti ya saa kati ya saa yako ya ndani na UTC (Saa Inayoratibiwa ya Kimataifa).

Nchi/Eneo:

Teua nchi au eneo ambalo unatumia kichapishi chako. Iwapo utabadilisha nchi au eneo, mipangilio yako ya faksi inarejea kwa chaguo-msingi na lazima uiteue tena.

Lugha/Language:

Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.

Muda wa Shughuli Umeisha:

Teua On ili kurejesha skrini ya kwanza wakati hakuna operesheni imetekelezwa kwa muda uliobainishwa.

Kibodi

Badillisha muundo wa kibodi kwenye skrini ya LCD.