/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Zana za Kusasisha Programu (EPSON Software Updater)

Zana za Kusasisha Programu (EPSON Software Updater)

EPSON Software Updater ni programu inayotafuta programu mpya na zilizosasishwa kwenye wavuti na kuzisakinisha. Pia unaweza kusasisha ngome na mwongozo wa kichapishi.

Kumbuka:

Programu endeshi za Windows Server hazikubaliwi.

Mbinu ya Usakinishaji

Pakua EPSON Software Updater kutoka kwenye tovuti ya Epson.

Iwapo unatumia kompyuta ya Windows na huwezi kupakua kuipakua kutoka kwenye tovuti, unaweza kuisakinisha kutoka kwenye diski ya programu iliyotolewa.

http://www.epson.com

Kuanzia kwenye Windows
  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Epson Software > EPSON Software Updater.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.

  • Windows 7/Windows Vista/Windows XP

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote au Programu > Epson Software > EPSON Software Updater.

Kumbuka:

Kadhalika, unaweza kuwasha EPSON Software Updater kwa kubofya ikoni ya kichapishi kwenye mwambaa kazi ulio kwenye eneo kazi, na kisha uteue Kisasisho cha Programu.

Kuanzia kwenye Mac OS

Teua Nenda > Programu > Epson Software > EPSON Software Updater.