Mwongozo wa Kuteua Skrini ya Picha (Mw'o Mmoja)

Hapa unaweza kutazama picha zilizokuzwa moja baada ya nyingine.Bonyeza kitufe cha au ili kutazama picha ya awali au inayofuata.Iwapo unataka kuonyesha picha bila ikoni, bonyeza kitufe cha .Bonyeza kitufe hiki tena ili kurejesha ikoni.

Huonyesha Teua Menyu ya Picha ambayo hukuruhusu kuteua picha kwa urahisi.

Huonyesha maelezo ya Exif kama vile tarehe ya kuchapisha au kasi ya kupiga picha.

Hukuza picha.Bonyeza kitufe cha + ili kuongeza ukubwa wa picha na ubonyeze vitufe vya ili kuonyesha sehemu unayotaka kuangalia.Bonyeza kitufe cha OK ili urejee kwenye mwonekano wa asili.Ukuzaji kwenye skrini hii hakubadilishi matokeo ya uchapishaji.

Huweka idadi ya machapisho kwa kudonoa kitufe cha - au +.