Kuchapisha Bahasha

Unaweza kuchapisha baadhi ya aina za bahasha.

Kwanza chapisha mchoro wa bahasha kwenye karatasi la ukubwa wa A4, na kisha uukunje ili kuunda bahasha.

  1. Weka karatasi yenye ukubwa wa A4 kwenye kichapishi.

  2. Teua Chapa mbalimbali kwenye paneli dhibiti.

    Ili kuteua kipengee, sogeza kulenga kwa kipengee kutumia vitufe vya , na kisha bonyeza kitufe cha OK.

  3. Teua Origami.

  4. Teua Bahasha ya origami.

  5. Teua ukubwa wa bahasha.

  6. Teua usanifu wa bahasha.

  7. Teua muundo wa bahasha.

  8. Teua iwapo unataka kuchapisha mistari ya mkunjo au la.

  9. Ingiza idadi ya nakala, na kisha ubonyeze kitufe cha .