Kuchapisha katika Miundo Mbalimbali

Unaweza kuchapisha picha kwenye kifaa cha kumbukumbu katika miundo mbalimbali kama vile 2-juu na 4-juu. Picha zinawekwa kiotomatiki.

  1. Weka karatasi katika kichapishi.

  2. Chomeka kadi ya kumbukumbu kwenye mpenyo wa kadi ya kumbukumbu wa kichapishi.

  3. Wakati ujumbe unaokuambia kuwa kupakia picha kumekamilika unaonyeshwa, donoa kitufe cha OK.

  4. Teua Chapisha Picha kwenye paneli dhibiti.

    Ili kuteua kipengee, sogeza kulenga kwa kipengee kutumia vitufe vya , na kisha bonyeza kitufe cha OK.

  5. Teua Chapa ya Mpangilio.

  6. Teua mpangilio.

  7. Unda mipangilio ya karatasi na chapisho.

  8. Bonyeza kitufe cha .

  9. Teua picha unayotakaa kuchapisha kwenye skrini ya kuteua picha.

  10. Teua Uhakiki na Uchapishaji.

  11. Bonyeza kitufe cha ili kuhariri picha inavyohitajika.

  12. Ingiza idadi ya nakala, na kisha ubonyeze kitufe cha .