/ Kunakili / Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili

Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili

Kumbuka:

Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.

Kuza:

Husanidi mgao wa ukuzaji wa upanuaji au upunguzaji. Iwapo unataka kupunguza au kuongeza ukubwa wa nakala asili kwa asilimia maalum, teua thamani, na kisha uingize asiliamia ndani ya kiwango cha 25 hadi 400%.

  • Saizi Halisi

    Hunakili kwa ukuzaji wa 100%.

  • A4→A5 na nyingine

    Hukuza au kupunguza nakala asili kiotomatiki ili kutoshea kwenye ukubwa wa karatasi bainifu.

  • Tosheza Ukrs Oto

    Hutambua eneo la kuchapisha na kukuza kiotomatiki au kupunguza nakala asili ili itoshee kwenye ukubwa wa karatasi uliyoteua. Wakati kuna pambizo nyeupe kwenye nakala asili, pambizo hizo nyeupe kutoka kwenye alama ya kona ya kioo cha kitambazaji zinatambuliwa kama eneo la kutambaza, lakini pambizo katika upande mkabala zinaweza kupunwa.

Ukubwa wa Karatasi:

Teua ukubwa wa karatasi uliyopakia.

Aina ya Karatasi:

Teua aina ya karatasi uliyopakia.

Mkanda wa Karatasi:

Angalia chanzo cha karatasi ambacho unataka kutumia.

Kurasa Nyingi:
  • Ukurasa Mmoja

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.

  • 2-juu

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mwelekeo na ukubwa wa nakala yako asili.

Ubora:

Teua ubora wa kuchapisha. Bora hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini.

Ondoa Mipangilio Yote:

Huweka upya mipangilio ya nakala kwa chaguo-msingi yake.